Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye leo Desemba 4, 2019 ametangaza kuondoka CHADEMA
Akiongea leo kwenye mkutanao wake na waandishi wa Habari katika ukumbi wa LAPF Makubusho jijini Dar es salaam , Fredrick Sumaye amesema ameamua kuondoka CHADEMA kutokana na figisu alizofanyiwa baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa.
Sumaye ameeleza kuwa alitaka kugombea nafasi ya Uenyekiti ili kuondoa dhana iliyopo miongoni mwa watu kua nafasi ya Mwenyekiti ndani ya CHADEMA ni ya Freeman Mbowe na haiguswi.