Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani na wenzake kutoka Jamhuri ya watu wa China wakimpima mtoto kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo Cardiogram) kabla ya kumfanyia upasuaji mdogo wa kuziba tundu la moyo kupitia mshipa wa damu wa kwenye paja kwa kutumia mashine ya (ECHO machine) bila ya kutumia mionzi (Transthoracic Echocardiography – TTE). Mara nyingi upasuaji huo hufanyika kwa njia ya mionzi kwa kutumia mtambo wa Cathlab (Catheterization Laboratory).
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Jamhuri ya watu wa China Prof. PAN Xiang Bin akimfanyia mtoto mwenye umri wa miaka minne ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) upasuaji mdogo wa kuziba tundu la moyo bila kufungua kifua kupitia mshipa wa damu wa kwenye paja kwa kutumia mashine ya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO machine) bila ya kutumia mionzi (Transthoracic Echocardiography – TTE). Mara nyingi upasuaji huo hufanyika kwa njia ya mionzi kwa kutumia mtambo wa Cathlab (Catheterization Laboratory).
Madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Jamhuri ya Watu wa China wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumfanyia mtoto upasuaji mdogo wa kuziba tundu la moyo bila kufungua kifua kupitia mshipa wa damu wa kwenye paja kwa kutumia mashine ya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO machine) bila ya kutumia mionzi (Transthoracic Echocardiography – TTE). Mara nyingi upasuaji huo hufanyika kwa njia ya mionzi kwa kutumia mtambo wa Cathlab (Catheterization Laboratory).
Picha na JKCI