Home Mchanganyiko JAMII IMETAKIWA KUACHANA NA BIASHARA HARAMU ZA MADAWA YA KULEVYA NA KUGUSHI...

JAMII IMETAKIWA KUACHANA NA BIASHARA HARAMU ZA MADAWA YA KULEVYA NA KUGUSHI NYARAKA ZA SERIKALI.

0

****************************************

Na farida saidy,morogoro

Jamii imetakiwa kuachana na biashara haramu za madawa ya kulevya
na kugushi nyaraka za serikali badala yake kufunya shughuli halali
ambazo zinaweza kuwaingizia kipato hususani katika kipindi hiki cha
kuelekea katika sikukuu za mwisho wa mwaka.

Lai hiyo imetolewa na kamanda wa polisi mkoa wa morogoro wilboad
William Mtafungwa ofisini kwake, baada ya watu tisa kukamatwa kwa
makosa tofauti yakiwemo kusafirisha madawa ya kulevya aina ya bhangi
na kugushi nyaraka za serikali pamoja na wizi wa thamani za dani
zikiwemo runinga.

Jeshi la polisi mkoa wa morogoro tunawashikilia watu tisa kwa
matukio mbalimbali ya uharifu pia tumefanikiwa kukamata bhangi
gunia 6,kg 6 na kete 50 ya bhangi, roli lililokuwa likisafirisha
bgangi,tv 08,computer 02 na pia tunaendelea na uchunguzi wa
matukio mbalimbali ya jinai yaliyojitokeza.alisema kamanda
mtafungwa.

Aidha amesema kuwa mnamo tarehe 30/11/2019 majira ya 00:30 katika
kijiji cha dala kata na tarafa ya mvuha askari polisi wakiwa doria
wamefanikiwa kuwakamata wasafirishaji bhangi kwa kutumia roli aina
ya fuso lenye namba T.671CPM.

Amesema Wasafirishaji hao ni Respice Joachimu deleva wa gali, Iddi
Boga utingo wa gali hilo, Abdalla Azizi bodaboda wote wakiwa wakazi
wa manispaa ya morogoro,ambapo walisafilisha bhangi hizo ndani yake
kukiwa na mfuko wa pumba za mpunga.

Katika hatua nyingine kamanda Mtafungwa amesema kuwa
wanamshikilia mkurugenzi wa kampuni ya MOROSIGN, Bwana omari Kassim Mataka na Bwana Mussa Salim Mshana afisa masoko wa
kampuni ya SUPER TECH ENTERPRISES kwa kosa la kukutwa na
vifaa vya kugushi nyaraka serikali zikiwemo za TRA na TANESCO.

Hata hivyo kamanda mtafungwa amewataka watanzania kuachana na
imani za kishirikina baina yao badala yake kutoa taarifa kwa jeshi la
polisi pale wanapoona kunawalakini katika jamii.