MKURUGENZI wa Halmashauri ya Pangani Issaya Mbenje akitoa hotuba yake wakati wa maadhimisho ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambapo kimkoa yaliyofanyika kwenye Kata ya Madanga wilayani Pangani mkoani Tanga kushoto mwenye miwani ni Ofisa Mradi wa Taasisi ya Mkapa Foundation Dkt Anastazia Masanja
Kaimu mratibu wa Huduma za VVU Mkoa wa Tanga Rose Kiluvia akitoa hotuba yake wakati wa maadhimisho hayo
Ofisa Mradi wa Taasisi ya Mkapa Foundation Dkt Anastazia Masanja akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
Upimaji magonjwa mbalimbali ukiendelea kwenye maadhimisho hayo
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Pangani Isaya Mbenje katika akiwa na awadau mbalimbali wakitoka kukagua moja ya mabanda yaliyopo kwenye viwanja ambavyo kulifanyika maadhimisho hayo
MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Isaya Mbenje kulia akiteta jambo Ofisa Mradi wa Taasisi ya Mkapa Foundation Dkt Anastazia Masanja mara baada ya kukagua mabanda
MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Isaya Mbenje kushoto akimsikiliza kwa umakini mmoja wa wataalamu wakati alipotembelea mabanda
TAASISI ya Mkapa Foundation imesema kwamba licha ya elimu kuhusu ugonjwa wa ukimwi kutolewa miaka mingi lakini jamii bado jamii haijabadilika katika suala zima la kuwanyanyapaa watu wanaishi na maambuzi wa virusi vya Ukimwi.
Hayo yalisemwa na Afisa Mradi wa Taasisi hiyo Dkt Anastazia Masanja wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambapo kimkoa yaliyofanyika kwenye Kata ya Madanga wilayani Pangani mkoani Tanga ambapo alisema hali hiyo imepelekea watu kuwa na hofu kipima afya zao kwa kuhofia kunyanyapaliwa.
Alisema changamoto ya unyanyapaaji pindi mtu anapobainika kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi imekuwa ni kubwa hasa katika wilaya za Handeni, Pangani na Kilindi huku akiitaka jamii kuachana navyo.
Ofisa huyo alisema tokea wameanza programu ya upimaji inayofahamika kama “Furaha yangu”wamefanikiwa kupima watu 45,515 katika kata 30 za wilaya hizo ambapo watu 708 walikutwa na maambukizo ya ugonjwa huo.
Awali akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Kaimu mratibu wa Huduma za VVU Mkoa wa Tanga Rose Kiluvia amesema katika Mkoa wa Tanga waliogunduliwa kuwa na VVU na Ukimwi tangu kipindi cha mwaka 2002 hadi 2019 ni 238,872 na watu 32,190 walikufa.
Naye kwa upande wake Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Issaya Mbenje, alisema ili kufikia asilimia 95 tatu ambayo ni lengo la serikali ifikapo 2030 kuhakikisha kiwango cha maambukizi kimepungua ifikapo mwaka huo.
Alisema tatizo la maambuzi ya VVU na Ukimwi ni kubwa na changamoto katika ya jamii ni maendeleo kwenye mkoa wetu wa Tanga na hiyo ni kulingana na matokeo ya utafiti wa kitaifa vya vuiashiri vya malaria na ukimwi vya mwaka 2017/2018.
Alisema viashiria hivyo vinaonyesha kiwango cha maambukizi ya kitaifa ni asilimia 5.1 na kwa mkoa wa Tanga hali ya maambukizi ni asilimia 5.0 maana yake kati ya watu 100 watu watano wana maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Taasisi hiyo ya Mkapa Foundation imeanza shughuli zake Julai mwaka 2018 katika wilaya za Pangani, Handeni na Kilindi lengo hasa ni kutoa elimu na kuifanya jamii kuwa na hamasa ya kuondokana na maambukizi mapya pamoja na jamii kujijengea utaratibu wa kupima afya zao.