Home Makala CECAFA BADO NI UCHOCHORO WA KANDA ZINGINE AFRIKA

CECAFA BADO NI UCHOCHORO WA KANDA ZINGINE AFRIKA

0

Na.Imani Kelvin Mbaga,Dar es Salaam

Hatua za mtoano katika michuano ya klabu barani Afrika zimekamilika jana, baada ya timu takribani 30 kupambana kutafuta tiketi 16 za hatua ya makundi katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Timu mbili za Esae na Generation Foot zitakamilisha idadi ya timu 16 baada ya michezo Yao kukamilisha watakapojitupa dimbani kuanzia kesho.

Katika hatua ya 32 iliyochezwa jana CECAFA iliingiza timu zake zisizopungua 5 ambapo zote zimekubali vipigo na kutupwa nje ya michuano hiyo.


Safari hii tutaishuhudia El-Hilal Omdurman pekee ikiiwakilisha CECAFA katika hatua ya makundi klabu bingwa Afrika.


Ukanda wetu unategemea zaidi bahati kuliko kanuni, mipango na mikakati katika maendeleo ya mpira.


Kwa miaka yote vilabu vyetu vimeendelea na utaratibu ule ule katika mambo ya msingi kama vile, uendeshaji wa ligi, uendeshaji wa vilabu, usajili, uimarishwaji wa benchi la ufundi nk.


Kwa bahati mbaya katika ukanda huu hutakiwi kusema ukweli bali ni kuwa shabiki, mnafiki na mtu wa mihemko kwa kurusha lawama kwa watu wasiohusika.


Jinsi unavyoona mashabiki mtandaoni ndivyo walivyo wanachama na VIONGOZI watakuwa hivyo hivyo kwakuwa hutoka miongoni mwao.
Kila mwaka tunaishia kuzomeana, kutimua makocha na kusajili upya bila ya kujifunza chochote.
Wadau wa soka, watalaam na wabobezi ktk soka wa ukanda wetu ni muhimu kukaa na kuchukua hatua za makusudi ili kulinusuru soka letu.
Robert Einstein mwanadamu anaedhaniwa kuwa na “IQ” kubwa kuliko wote aliwahi kusema “upumbavu” ni kufanya jambo lile lile, kwa namna ile ile huku ukitegemea matokeo tofauti, tujitahidi Kujiondoa kwenye upumbavu huu kwakuwa wanaoumia zaidi ktk mfumo huu ni wale wanaojua njia sahihi na hawaoni ikitendeka.


Tumerudi wote kwenye ligi zetu, tuje tucheze, tuzomeane, tutukane waamuzi na makocha, tuondoe VIONGOZI madatakani, tutazane faini kisha mwakani miezi kama hii tutegemee kuwa tishio Afrika “what a shame”
CECAFA tutaendelea kuwa “underdog”?