*******************************
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Eng. Stellah Manyanya amezitaka idara mbalimbali za Serikali kuipa kipaumbele sekta ya ardhi katika mipango ya maendeleo inayofanyika nchini.
Eng. Stellah Manyanya ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano mkuu wa sita wa Mwaka wa Wataalaamu wa Mipangomiji ulioanza tarehe 27 hadi 29 Novemba 2019 jijini Dodoma.
Eng. Stellah Manyanya amesema, kumekuwepo na miradi mingi nchini inaanzishwa na Serikali inatumia gharama kubwa katika kuikamilisha matokeo yake imekuwa haitumiki na wakati mwingine inaingiliana na shughuri nyingine za kijamii hali inayopelekea kuzuka kwa migogoro katika jamii.
Akitolea mfano Jengo la Machinga Complex lililopo Ilala Jijini Dar es Salaam, Eng. Stellah Manyanya amesema kuwa kutokuwepo kwa mipango kina ya muda mrefu na utafiti duni ndio chanzo kikubwa hadi leo hii jengo hilo kushindwa kufikia lengo walilojiwekea la kuwa saidia wafanyabiashara wadogowadogo kuwa na sehemu yao ya kufanyia shughuri zao.