Home Mchanganyiko MTAA WA CHUO KIKUU WAPATA VIONGOZI WAPYA

MTAA WA CHUO KIKUU WAPATA VIONGOZI WAPYA

0

Huu ni uongozi mpya wa Mtaa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwenyekiti Dr. Jonas Tiboroha ( wa nne kutoka kushoto) pamoja na wajumbe wake.

*******************************

Viongozi wa Serika ya Mtaa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wameapishwa leo katika ukumbi wa Urafiki Social Hall  Ubungo leo tarehe 29/11/2019  na kuahidi kufanya mabadiliko makubwa ya kimaendeleo  katika mtaa wao ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuri   inayotaka wananchi  kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kufikia maendeleo ya uchumi wa kati. Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa mtaa huo Dr. Jonas Benedict Tiboroha mara baada ya kuapishwa.

Amesema kazi ya kuwatumikia wananchi wa Mtaa wake imeishaanza hivyo basi wategemee mabadiliko pamoja na maendeleo. Anawaomba ushirikiano kwani kupitia ushirikiano utaleta chachu ya maendeleo.