Afisa uhamiaji akihudumia Mwananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada uliofanyika Mji mdogo wa Makambako.
Kampuni za simu wakisajili Wananchi wa Mji Mdogo wa Makambako laini za simu kwa alama za vidole.
Wananchi wakipata huduma ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika Mji Mdogo wa Makambako.
*************************************
Kufuatia na kujitokeza kwa wingi kwa wakazi wa Makambako na viunga vyake vya jirani katika zoezi la kupata namba za vitambulisho vya taifa na kusajili simu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kushirikiana na Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA na watoa huduma wote wa makampuni ya simu wameongeza muda wa zoezi hilo ambapo sasa zoezi hilo utafanyika kwa wiki nzima kuanzia Desemba 2 hadi 6 2019.
Akizungumzia maendeleo ya zoezi hilo linaloratibiwa na TCRA mkuu wa kanda ya Nyanda za juu Kusini Mhandisi Asajile John amesema lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wanaopata huduma za msingi kwa urahisi hivyo kuongeza huko kwa siku kunalenga kutekeleza malengo hayo.
Amesema huo ni muendelezo wa kampeni ya “Mnada kwa Mnada, Karibu tukuhudumie” iliyoanzishwa na kuratibiwa na TCRA na kushirikisha wadau wengine inayolenga kutoa elimu ya utumiaji bora na salama wa huduma za mawasiliano na kuhamasisha usajili wa laini kwa kutumia namba za vitambulisho vya taifa.