Na.Farida Saidy,Morogoro
…………………….
Wakala Wa Usajili Ufilisi Na Udhamini (RITA) Kupitia Wasajili Wa Huduma Ya Uandikishaji Watoto Chini Ya Umri Wa Miaka Mitano Wametakiwa Kutofanya Urasimu wa kuwatoza Watu Fedha kwa ajiri ya malipo ya ya cheti cha kuzaliwa, Ikiwa Mkakati Uliopo sasa Ni Kusajiliwa Bure, Na Kwa Atakaebainika Kufanya Hivyo Hatua Kali za kisheria Zitachukuliwa Dhidi Yake.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Mkuu Wa Mkoa Wa Mororgoro Bw.Loata Ole Sanare Wakati Wa Ufunguzi Wa Semina Ya Wakala Wa Usajili Ufilisi Na Udhamini (RITA) Uliowahusisha Viongozi Mbalimbali Wa Kimkoa Wenye Dira Ya Kufikia Lengo La Kusajili Watoto Zaidi Y Asilimia 90 Ya Watoto Wote Bure , Wenye Umri Chini Ya Miaka Mitano Mkoani Morogoro.
Kwa Upande Wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Kutoka RITA Bi. Emmy Hudson Amesema Ili Kukamilisha Majukumu Kwa Watendaji Kuhusu Mpango Huo,Wameandaa Mafunzo Kwa Wahusika Wote ,Wakiwemo Watumishi Sita Kutoka Kila Halmashauri Mkoani Morogoro ,Pamoja Na Mtumishi Mmoja Mmoja Kutoka Idara Ya Usalama Na Idara Ya Uhamiaji .
Nao Baadhi Ya Washiriki Wa Semina Hiyo Wakiwemo Viongozi Mbalimbali Wa Kiserikali Na Kidini Wameusifu Mpango Huo Wa Usajili Bure Wa Watoto Wenye Umri Chini Ya Miaka Mitano Unaoendelea Kuifikia Mikoa Mbali Mbali Nchini Na Kusema Kuwa Utawasaidia Katika Kuharakisha Upatikanaji Wa Haraka Wa Vyeti Hivyo.
Ikumbukwe Kuwa Kundi La Awali La Watoto Walio Chini Ya Umri Wa Miaka Mitano Limekwishaanza Utekelezaji Wake Ambapo Ni Mikoa Ya Mbeya Songwe Mwanza Njombe Iringa Geita Shinyanga Lindi Mtwara Mara Simiyu Dodoma Na Singida Ambapo Kwa Sasa Ni Zamu Ya Morogoro Pamoja Na Pwani.