Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin kunambi,akizungumza na viongozi wapya wa serikali za mitaa waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Novemba 24,2019 mara baada ya kuwaapisha leo.
Sehemu ya viongozi wapya wa serikali za mitaa waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Novemba 24,2019,akila kiapo mara baada ya kuwaapisha leo na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin kunambi
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin kunambi,akifafanua jambo kwa viongozi wapya wa serikali za mitaa waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Novemba 24,2019 mara baada ya kuwaapisha leo.
…………………
Na.Alex Sonna,Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Godwin kunambi amewataka viongozi wapya waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa hivi karibuni kuachana na tabia ya kujali maslahi yao binafsi badala yake waende kutenda haki kwa wananchi waliowachagua na kwa kufanya hivyo itasawaidia kuaminika kwa wananchi.
Kunambi ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akiwaapisha viongozi wapya wa serikali za mitaa ambao walichaguliwa Novemba 24,2019.
Mhe.Kunambi amesema kuwa watakuwa na utaratibu wa kutoa tuzo kwa mitaa kumi kila baada ya miezi sita katika Jiji la Dodoma kwani wanahitaji kuwa na mfumo shirikishi kwa wananchi ili kila mwananchi katika mtaa wake awe sehemu ya kusimamia sheria na taratibu zilizowekwa na serikali.
Hata hivyo,amewataka viongozi hao wapya kutojikita kwenye tabia ya kuwatoza fedha wananchi pindi wanapohitaji huduma ya mihuri huku wakiaswa pia kutokuwa chanzo cha kuzalisha migogoro katika maeneo yao.
Awali akitoa taarifa fupi ya mwenendo wa uchaguzi wa serikali za mitaa katka jiji la Dodoma ulifanyika November 24,2019 Msimamizi wa uchaguzi Dikson Kimaro ,amesema mitaa yote katika jiji la Dodoma iliweza kushiriki katika hatua za awali za uchaguzi ambapo vyama vilivyoonesha kushiriki uchaguzi huo ilikuwa ni chama cha mapinduzi CCM,ACT WAZALENDO,CHADEMA,Alience for African formers party AFP, Chama cha wananchi CUF,Chama cha umma CHAUMA pamoja na chama cha Demokrasia Makini .
Aidha Bw.Kimaro amesema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka huu ulisimamiwa na kuendeshwa kwa kufuata sheria,kanuni za mitaa ngazi ya vijiji,vitongoji na mitaa za mwaka 2019 na miongozo ya uchaguzi wa serikali za mitaa iliyotolewa na ofisi ya Rais TAMISEMI .
Mwenyekiti wa Kata ya Kilimani mtaa wa chinyoya Bw.Faustine Bendera aliye apishwa amesema kuwa kikubwa nikwenda kuwatumikia wananchi kwa moyo wote ilikuendana na kazi ya Rais
“kikubwa ni kujituma n wananchi watarajie maendeleo na tunachoomba ni ushirikiano maana hatuwezi kufanya lolote pasipoi ushirikiano wa wananchi”amesema Bendera
Viongozi hao wa halmashauli ya jiji la Dodoma wameapishwa ambao ni wenyeviti wa mitaa 222 nafasi za wanawake 444 na nafasi za mchanganyiko 666.