MKUU wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Yonna Mark akizungumza wakati akifungua mkutano wafanyabiashara eneo la Horohoro wilayani Mkinga ulioandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Tanga ikiwa ni kutoa elimu juu ya umuhimu wa wao kulipa kodi kwa hiari kulia ni Afisa Mfawidhi wa Forodha wa TRA Horohoro Bakari Athmani na Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria kushoto ni Meneja wa TRA wilaya za Muheza na MkingaDaudi Njohole
Meneja wa TRA wilaya za Muheza na MkingaDaudi Njohole akizungumza wakati wa mkutano huo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark akifuatiliwa na Afisa Mfawidhi Forodha wa TRA Horohoro Bakari Athmani na Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria
Afisa Mfawidhi wa Forodha wa TRA Horohoro Bakari Athmani akizungumza kulia ni Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark
Afisa Elimu Mlipa Kodi wa TRA mkoani Tanga Salim Bakar akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
Afisa Elimu Mlipa Kodi wa TRA mkoani Tanga Salim Bakar akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria akieleza jambo katika mkutano huo
Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa kwenye mkutano huo
MKUU wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Yona Mark amewaonya wenyeviti wapya wa vijiji na vitongoji wilayani humo kuacha kujshughulisha na biashara za magendo badala yake wawe ndio walinzi wa kuwafichua wahusika ili kukomesha vitendo hivyo.
Mark aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wafanyabiashara eneo la Horohoro wilayani Mkinga ulioandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Tanga ikiwa ni kutoa elimu juu ya umuhimu wa wao kulipa kodi kwa hiari.
Alisema kutokana na wilaya hiyo kuwa mpakani mwa nchi ya Kenya hivyo ikiwemo ukanda wa bahari na nchi kavu hivyo upo uwezekano wa vitendo vya namna hivyo kufanya huku akiwataka viongozi hao kuvikemea na kutokuviruhusu kwenye maeneo yao.
“Ndugu zangu wevyeviti wa vijiji na vitongoji acheni kushirikia kwenye vitendo vya biashara za magendo kwani kufanya hivyo tunaikosesha serikali mapato yake ambayo yangesaidia kuchochea shughuli za kimaendeleo lakini pia niwaambie kwamba tutakaobaini tutashughulikiwa kwa mujibu wa sheria”Alisema Mkuu huyo wa wilaya
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba wataendelea kushirikiana na TRA kufanya operesheni za kupambana na vitendo vya biashara haramu za magendo ili kuvikomesha kabisa kwani kutoka Tanga mpaka mpakani eneo la Horohoro wana kilomita 70 za maji hivyo kupambana na hilo wataanzisha bandari ndogo eneo la moa wilayani Mkinga.
Alisema kwamba wanaanzisha ili kuiwezesha serikali kupata kodi huku akieleza wanatarajia kulifanya hilo miezi michache ijayo watakuwa wamekwisha kufungua huku akiwataka wafanyabiashara hao kutumia njia halali za kupisha bidhaa zao badala ya zile za panya.
,dc akizungumzia mashine za EFD alisema zinawasaidia wafanyabiashara kutokana na kwamba zinaweka mahesabu yao vizuri kutokana na kwamba kila kinachouxwa kinaonekana.hata hivyo aliwataka wafanyabiashara kutangaza biashara zao ili ziweze kutambulika na hatimaye kuweza kupata wateja na hatimaye kuwza kuingiza kipato.ulipaji wa kodi
Awali akizungumza Afisa Elimu Mlipa Kodi wa TRA mkoani Tanga Salim Bakar alisema kwamba hivi sasa walipa kodi wanatambua umuhimu wa kulipa kodi kutokana na Serikali ya awamu ya tano kutekeleza mambo kwa vitendo na kuonekana maendeleo mbalimbali ikiwemo madawa, elimu bure na miradi mbalimbali inatekelezwa kupitia kodi hizo.
Naye kwa upande wake ,Diwani wa Kata ya Duga (CCM) Ally Ally amesema umuhimu wa kulipa kodi kwa wananchi ni mkubwa kutokana na kwamba maendeleo yanayopatikana yanatokana na uwepo wa ulipaji wa kodi hizo.
“Mimi kama diwani wa Kata ya Duga nitaendelea kuhakikisha ninahamasisha wananchi kuendelea kulipa kodi kwa lengo la kusaidia kuchochea kasi ya ukuaji wa maendeleo “Alisema
Hata hivyo pia Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria aliwataka wafanyabiashara kuhakikisha wanalipa kodi kwa hiari ili kuwasaidia ukuaji wa maendeleo.
“Kwani wafanyabiashara kulipa kodi ndio Taifa linaendelea lakini pia kuchochea ukuaji wa maendeleo lakini pia hakikisheni mnatoa risiti wakati mnapouza bidhaa zenu “Alisema