Home Michezo YANGA YAJIPANGA KUIKABILI ALLIANCE FC HAPO KESHO KUTWA

YANGA YAJIPANGA KUIKABILI ALLIANCE FC HAPO KESHO KUTWA

0

************************************

Klabu ya Yanga ambayo leo hii asubuhi imetua jijini Mwanza kwaajili ya mechi yao dhidi ya Alliance Fc hapo keshokutwa, imeweka kambi tayari mkoani Mwanza leo kwa ajili ya kujiaandaa na mchezo huo.

Yanga itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-2 mbele ya JKT Tanzania huku Alliance FC ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa kufungwa mabao 5-0 dhidi ya Azam FC uwanja wa Nyamagana,

Kocha wa muda ya Yanga Charlse Mkwasa amesema kuwa kikosi kipo sawa na morali ni kubwa kwa ajili ya mchezo huo muhimu.

“Mchezo wetu utakuwa mkubwa na mgumu hivyo tutawafuata wapinzani wetu tukiwa na tahadhari kubwa ili kupata matokeo chanya,” amesema Mkwasa