Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na tukio la Daktari wa Hospitali ya Chake chake aliekamatwa kwa tuhuma za kuomba Rushwa ya Ngono hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Waziri wa afya kuzungumzia tukio la Daktari wa Hospitali ya Chake chake aliekamatwa kwa tuhuma za kuomba Rushwa ya Ngono hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
**************************************
Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar 26/11/2019
Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohammed amewataka wagonjwa kutoa taaarifa wanapofikwa na jambo la udhalilishaji.
Ameyasema hayo huko Ofisini kwake Wizara ya afya, wakati akitoa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na taarifa ya daktari wa Hospitali ya Chake kutaka rushwa ya ngono kwa mgonjwa.
Amesema kitendo hicho sio kizuri kwa taifa kwani kinawafanya wagonjwa kuwa na wasiwasi ambao wanapohitaji matibabu wakati wanapofika hospitali.
Aidha amesema Serikali haikufurahishwa na kitendo hicho hivyo kwa kushirikina na Wizara ya Afya wamechukua hatua ya kumtaka muhusika kutoa taarifa ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Pia Mhe. Hamad amesema katika kupambana na tatizo hilo Serikali imeamua kumsimamisha kazi daktari huyo ili kupitisha uchunguzi na kuchukua hatua za sheria ikiwa atathibitishwa kufanya udhalilishaji huo .
Hata hivyo Waziri huyo amewataka akina baba kushirikiana na wake zao wakati wanapokwenda Hospitali kimatibabu ili kuepuka vitendo vya udhalilishaji .
Akizungumzia suala la mshahara kuhusu daktari huyo Mkurugenzi Mtendaji Utumishi Wizara ya afya Ramadhan Khamis Juma amesema kwa sasa analipwa nusu mshahara hadi kukamilika uchunguzi na ikigundulika kufanya hivyo atasimamishiwa mshahara wake.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO