Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongozana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi , Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu) Andrew Massawe (Kulia) na kushoto kwake Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Hosea Kashimba, kukagua Nyumba za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi , Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu) Andrew Massawe wakati alipokagua Nyumba za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam.
Baadhi ya Maofisa ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), wakifuatilia nyaraka za nyumba Nyumba za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na mmoja wa waliofanikiwa kununua Nyumba za gharama nafuu za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na mmoja wa waliofanikiwa kununua Nyumba za gharama nafuu za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na mkazi wa Buyuni, Benjamini Mvungi wakati alipokagua Nyumba za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam.
*****************************
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama leo tarehe 26 Novemba, 2019 anatarajia kutangaza utaratibu mpya wa kununua Nyumba za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam.
Akiongea mara baada ya kumaliza kukagua mradi huo wa nyumba zinazomilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), tarehe 25 Novemba 2019, Mhe. Mhagama amebainisha kuwa lro atatoa utaratibu huo mpya wa namna ya kununua nyumba hizo zilizo wazi ili wananchi waweze kunufaika kwa kupata makazi bora na salama.
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), unaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, na umeanzishwa na Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2018, Jukumu kuu la mfuko huo ni kukusanya michango na kulipa mafao ya kustaafu kwa watumishi wa umma.