Bishop Flaston Ndabila (kulia) na Mke wake Janeth Ndabila wa Kanisa la ABC Tabata waandaaji wa Kongamano na Tamasha la Uimbaji wakiwa katika picha ya pamoja. Tamasha hilo litakwenda sanjari na kuwapongeza wanandoa hao kwa kutimiza miaka 25 ya ndoa, miaka 25 ya huduma na miaka 50 ya kuzaliwa.
Bishop Mark Mugekenyi Kairuki (Kenya)
Bishop Mussa Ngobese (Afrika Kusini)
Pastor Fred Msungu (Tanzania)
Pastor Harerimana Tharcise (Burundi)
Bishop Robson Simkoko (Malawi)
Apostle Moses Silwamba (Zambia)
Na Dotto Mwaibale
KONGAMANO na Tamasha la Uimbaji wa nyimbo za injili linatarajia kufanyanyika kwa siku tatu mfululizo katika Kanisa la ABC lililopo Tabata Mandela Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Mratibu wa Tamasha hilo Askofu Flaston Ndabila alisema maandalizi yote ya kongamano na tamasha hilo litakalo anza Desemba 6, 2019 yamekamilika.
” Maandalizi yote ya tamasha letu yamekwisha
kamilika na wageni tulio waalika kutoka ndani na nje ya nchi wamethibitisha kuja kushiriki” alisema Ndabila.
Alisema kwamba katika kongamano na tamasha hilo kutakuwa na mafundisho ya ndoa na familia ambayo yatafanyika Desemba 7, Ibada ya shukurani ambayoitafanyika Desemba 8 na kuhitimishwa na kilele cha furaha Desemba 9, 2019.
Askofu Ndabila aliwataja watumishi wa mungu watakaoshiriki katika kongamano hilo kuwa ni Bishop Mark Mugekenyi Kairuki (Kenya) Bishop Mussa Ngobese (Afrika Kusini) Apostle Moses Silwamba (Zambia) Pastor Harerimana Tharcise (Burundi) Pastor Fred Msungu (Tanzania) Bishop Robson Simkoko (Malawi) na Mimstori: Eliya Mwaitondo wa Tanzania.
Alisema Kongamano hilo litaanza kanisani hapo kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 12 jioni kila siku na kuwa watu wote wanakaribishwa na kwa maelezo zaidi ya kushiriki unaweza kupiga simu namba 0754 762301 na 0715684590.