**************************************
Na Tito Mselem, Bukombe
Waziri wa Madini Doto Biteko ametoa mifuko 100 ya saruji pamoja na mbao zenye htamani ya Shilingi milioni 4.2 ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya cha Imalanguzu Wilayani Bukombe Mkoani Geita.
Waziri Biteko ametoa mchango huo ili kutatua changamoto ya huduma za afya katika Kijiji cha Imalanguzu Wilayani Bukombe ambapo huduma hizo zimekuwa kikwazo kwa wakazi wa Kijiji wa Kijiji hicho kwa muda mrefu.
Waziri Biteko ametatua changamoto hiyo alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi na kufanya mkutano wa hadhara katika Kijiji hicho na kubaini mapungufu makubwa katika sekta ya afya Wilayani humo.
Aidha, Waziri Biteko, amewapongeza Walimu wote wa Wilaya ya Bukombe kwa ushindi mkubwa walioupata baada ya Wilaya hiyo kuongoza katika ufaulu wa darasa la saba kimkoa na kushika nafasi ya 27 kitaifa kati ya shule 188.
Wakati huo huo, Waziri Biteko, ametoa rai kwa wananchi wa Imalanguzu kuhakisha wanapeleka watoto wao shule kwani ndiyo urithi pekee ambao unaweza kumuachia mtoto na baadae ukamsadia.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anatoa kila mwezi zaidi ya shilingi bilioni 27 ili watoto wetu wasome bule na nchi hii inahitaji wasomi wengi ili walisaidi taifa hili, nitashangaa sana nikisikia mzazi hajampeleka mtoto wake shule,” alisema Biteko.
Pamoja na hayo, Waziri Biteko amewaasa wanafunzi wote Wilayani humo kutekeleze wajibu wao wa kusoma kwa bidii na mara baada ya kumaliza elimu zao na kupata kazi wasiwasahau wazazi wao waliowapeleka shule badala yake waachane na zana ya kuwatelekeza wazazi wao ili wahudumiwe na TASAF.
Katika hatua nyingine, Waziri Biteko, amempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa hatua za kukuza uchumi wa nchi katika maeneo mbalimbali ikiwemo sekta ya madini, viwanda, afya na kilimo.
“Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa maendeleo aliyoyaleta, amejenga Reli ya kisasa, amenunu ndege zakutosha na ameanzisha miradi mikubwa mingi ambayo nimafanikio makubwa katika taifa letu, tumuunge mkono Rais wetu,”.
Pia, Waziri Biteko, amewasisitiza wananchi Wilayani Bukombe kuhakikisha wanafanya kazi ili waibadirishe Wilaya ya Bukombe iwe Bukombe mpya na yenye mafanikio, wasikubali kudanganywa kwamba maendeleo yataletwa na Serikali badala yake wafanye kazi wakishirikiana na Serikali ndiyo maendeleo yakuja.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bukombe Rozaria Masokola, amempongeza Waziri Biteko kwa msaada alioutoa katika kuhakikisha changamoto ya kituo cha afya katika Kijiji cha Imalanguzu inakuwa historia.