Home Michezo Waziri Dkt.Mwakyembe amekutana na uongozi na wachezaji wa timu ya Boma fc

Waziri Dkt.Mwakyembe amekutana na uongozi na wachezaji wa timu ya Boma fc

0

*******************************************

Mbunge wa Kyela na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) leo jioni amekutana na Uongozi na wachezaji wa Boma FC katika viunga vya Matema Beach Resort.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Wilaya ya Kyela ndugu Widrey Mwasyika, Mwenyekiti wa timu Gabriel Kipija, Katibu wa timu, Mpoki Mwaifunga pamoja na viongozi wengine wa timu.

Dkt. Mwakyembe amepokea taarifa ya timu na pia akazungumza na wachezaji kuhusu fursa na changamoto zilizopo katika timu. Dkt. Mwakyembe akizungumza katika kikao hicho amesema wakati umefika sasa kwa timu ya Boma kuboresha mfumo wake wa uendeshaji kuwa wa kampuni ili kuwezesha uwekezaji wa wadau mbalimbali.

Aidha, Dkt. Mwakyembe amesema ataendelea kuisaidia Boma FC katika jitihada za kufika Ligi Kuu. Dkt. Mwakyembe amesema pia ataendelea kuunga mkono zoezi la ukarabati wa Uwanja wa Mpira wa John Mwakangale ili uwe wa kisasa.
Dkt. Mwakyembe ameipatia timu ya Boma seti moja ya jezi, mipira miwili na fedha taslim