Home Mchanganyiko Wagombea 1,851 wa vyama vya upinzani kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa...

Wagombea 1,851 wa vyama vya upinzani kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Mkoani Rukwa.

0

********************************

Wagombea wa vyama vya upinzani wapatao 1,851 kushiriki katika nafasi mbalimbali za uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika nchini tarehe 24.11.2019 ili kuwapata wawakilishi katika ngazi ya kijiji, mtaa, kitongoji pamoja na wajumbe mchanganyiko na wajumbe wa viti maalum katika ngazi hizo.

Taarifa kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa inasema kuwa wagombea hao hawatakuwa na uwezo wa kuweka mawakala kisheria kwasababu mawakala hao wanatakiwa kuwa na kiapo cha kisheria pamoja na utambulisho kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi na kuongeza kuwa ni isipokuwa mgombea mwenyewe ndiye anaweza kuwa wakala.

Aidha, ametahadharisha kuwa endao kutatokea vurugu katika maeneo ambayo kwasababu nembo ya chama cha upinzani imetumika wakati mgombea amejitoa ambapo yawezekana alijitoa kwa kuchelewa au aliamua kutosumbuka kujitoa,Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya zitaimarisha ulinzi katika maeneo ya kupiga kura.

Idadi ya wagombea wa vyama vya upinzani waliobakia Mkoani Rukwa baada ya mwisho wa tarehe ya kujitoa 16.11.2019 saa 10 jioni ni katika vijiji 67 (19.7%), Vitongoji 348 (19.1)%, mitaa 9 (5.4%), wajumbe mchanganyiko 876 (11.8%) na wajumbe wa viti maalumu 551 (19.1%). Mkoa una jumla ya vijiji 339, vitongoji 1,817, mitaa165. Wajumbe mchanganyiko 7,420 na wajumbe wa viti maalum 2,875.

 Maelezo ya Picha

DSC_0205 – Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakimsikiliza Msimamizi wa Uchaguzi wa serikali za mitaa manispaa ya Sumbawanga Andre Zumba (kushoto) wakati akiwaonesha mfano wa karatasi ya kupigia kura siku ya tarehe 24.11.2019.