Katibu Tawala (RAS) wa mkoa wa Tanga, Zena Said akizungumza wakati akifungua mafunzo kuhusu Program ya Kuendeleza Mnyororo wa Thamani ya Mazao ya Misitu (FORVAC) yaliyofanyika mkoani hapo jana.Kulia ni Mratibu wa Program ya FORVAC, Emmanuel Msofe
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Zena Said akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mkutano kuhusu umuhimu wa waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuelimisha wananchi faida za utunzaji wa misitu.
………………….
NA SULEIMAN MSUYA, TANGA
KATIBU Tawala (RAS) wa mkoa wa Tanga, Zena Saidi amesema ili kupunguza upotevu na uharibifu wa rasilimali misitu ni lazima jamii inayozungukwa na misitu iweze kunufaika kiuchumi, kijamii na maendeleo.
Said aliyasema hayo jijini hapa wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu Program ya Kuendeleza Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Misitu (FORVAC).
Alisema mafunzo hayo ya mradi wa FORVAC kwa waandishi wa habari ni muhimu katika kuhakikisha jamii inapata ufahamu kuhusu faida ya rasilimali misitu.
Katibu misitu inaweza kuwa endelevu iwapo dhana nzima ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu (USM) inaonekana katika matokeo chanya.
Alisema misitu inaweza kutumiwa bila kuharibika kwa kuhamasisha kilimo rafiki na misitu kama kilimo cha iliki, pilipili mannga, kufuga nyuki na shughuli nyingine rafiki.
“Misitu ikitunzwa kwa mfumo shirikishi itaweza kuwa na matokeo chanya. Ila hilo litawezekana iwapo waandishi wa habari watashirikiana na kada zote kuelimisha,” alisema.
Katibu tawala huyo alisema elimu ya USM inapaswa kusambazwa nchi nzima na waandishi wa habari ndio chanzo muhimu.
Said alisema mkoa wa Tanga utunzaji wa mazingira upo vizuri hali ambayo inasadie upatikanaji wa maji kuwa wa uhakika.
Alisema wapo baadhi ya watu walitaka kuharibu msitu wa Amani Muheza lakini kwa sasa wamewadhibiti huku wakihamasisha upandaji wa miti ili misitu iwe endelelevu.
Katibu tawala aliwataka watekelezaji wa miradi kutumia lugha rahisi wanapoelezea miradi hiyo ili kurahisisha ujumbe unaofikia waandishi.
Alisema takwimu zinaonesha kwa mwaka Tanzania inapoteza hekta zaidi ya 469,000 huvyo ni vema zikawepo jitihada za utunzaji wa misitu.
Mratibu wa Program wa FORVAC, Emmanuel Msofe alisema wamelazimika kutoa mafunzo kwa vyombo vya habari ili waweze kuulewa mradi na kuelimisha jamii.
Msofe alisema program hiyo inatelelezwa katika wilaya 10 za Handeni, Kilindi, Mpwapwa, Liwale, Ruangwa, Nachingwea, Mbinga, Namtumbo, Songea na Nyasa.
“Nikiwaona nyie wanahabari nawaona Watanzania milioni 53 kwani madhumuni ya program ni kuona jamii inanufaika na kupata taarifa,” alisema.
Alisema program hiyo inagusa uchumi, jamii na maendeleo kupitia rasilimali misitu bila kusababisha uharibifu.
“Tunaongeza thamani ya mazao ya misitu, kujengea uwezo wadau kwa maana teknolojia na ujuzi, ugani, taarifa, sheria, Sera na miongozo mbalimbali,” alisema.
Kwa upande wake Mratibu wa Program Kanda ya Tanga, Petro Masolwe alisema mradi huo ulionza mwaka 2018 umeweza kuongeza mnyororo wa thamani katika maeneo yenye mradi.
Masolwa alisema baadhi ya nchi duniani ikiwe Finland zimeendelea kupitia misitu hivyo Tanzania inapaswa kutumia rasilimali hiyo kuchochea maendeleo.
“Pamoja na kupigania program hiyo waandishi wanapaswa kuandika kuhusu kampeni ya upandaji miti nchini kote. Tutaweza kupunguza uharibifu NA uootevu wa misitu,” alisema