Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa na Balozi wa Canada nchini Mhe.Pamela O’Donnell walipokutana kwa mazungumzo Ofisi za Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza na Balozi wa Canada nchini Mhe.Pamela O’Donnell alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dodoma
Balozi wa Canada nchini Mhe.Pamela O’Donnell akizungumza alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi patika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.
………………….
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O’Donnell ofisini kwake jijini Dodoma
Prof. Kabudi na Mgeni wake wamezungumzia namna ya kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Canada kwa manufaa ya nchi zao.
Prof. Kabudi amempongeza Mhe. Balozi kwa Canada kuendelea kuwa rafiki mzuri wa Tanzania na kumtaka kuendeleza urafiki huo.
Amesema kazi kubwa na nzuri ya kupambana na rushwa na ubadhirifu wa fedha na mali za umma inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inalenga kuwapatia maisha bora watanzania na hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa Kati na wa viwanda.
Naye Balozi O’Donell amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Tanzania ya kuimarisha ukuaji wa Uchumi, utoaji wa huduma bora za afya, elimu ya msingi bure kwa watoto wa kitanzania na uboreshaji wa miundimbinu kwa maendeleo ya Tanzania