Waandishi wa habari wakifuatilia mjadala katika mkutano uliowakutanisha waandishi wa habari,TAKUKURU pamoja na WFT kujadili ni namna gani wanaweza kupunguza athari zinazojitokeza maofisini pamoja na shuleni kuhusu suala la Rushwa ya Ngono.
Bi.Sarah Chodata kutoka ofisi ya kugurugenzi ya Elimu kwa Umma TAKUKURU, akizungumza mkutano uliowakutanisha waandishi wa habari kujadili ni namna gani wanaweza kupunguza athari zinazojitokeza maofisini pamoja na shuleni kuhusu suala la Rushwa ya Ngono.
Mkurugenzi Mtendaji wa Women Fund Tanzania(WFT), Bi.Merry Lusimbi akizungumza katika mkutano uliowakutanisha waandishi wa habari kujadili ni namna gani wanaweza kupunguza athari zinazojitokeza maofisini pamoja na shuleni kuhusu suala la Rushwa ya Ngono.
**********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Waandishi wa habari na wadau mbalimbali wametakiwa kupaza sauti juu ya maswala ya Rushwa hususani Rushwa ya ngono ili kuhakikisha jamii inajengewa uelewa na kuweza kupambana na janga hilo linaloenda kwa kasi zaidi nchini.
Akizungumza katika kikao kazi TAKUKURU pamoja na waandishi wa habari pamoja na wadau kutoka Women Fund Tanzania (WFT), Mwanasheria wa TAKUKURU Bw.IMANI NITUME amesema kuwa kumekuwepo na malalamiko mengi kuhusu maswala ya Rushwa ya ngono lakini bado hakuna takwimu rasimi zinazoonyesha ukubwa wa tatizo hilo.
“Mnamo mwaka 2018 kulifanywa marekebisho ya sheria ya Rushwa ya ngono na kuilifanya kosa hilo kuwa jina ambalo linajumuishwa katika makosa ya uhujumu uchumi ambapo adhabu yake ni kifungo cha miaka 20”.Amesema Bw.Nitume.
Kwa upande wake kutoka Mkurugenzi Mtendaji wa Women Fund Tanzania(WFT), Bi.Merry Lusimbi amesema kunatakiwa wadau wanatakiwa kujenga hoja zitakazoendana na na mikakati ya kampeni zitakazobeba sauti za waaathirika.
Nae Bi.Sarah Chodata kutoka ofisi ya kugurugenzi ya Elimu kwa Umma TAKUKURU, amesema tafiti zinapaswa kuendelea kufanyika katika jamii ili kuweza kubaini ukubwa wa tataizo hilo.