******************************
Dodoma- 21 Novemba, 2019
Mhe. Innocent L. Bashungwa, Waziri wa Viwanda na Biashara amemteua Bi. Loy
Waston Mhando kukaimu nafasi ya Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Usajili wa
Biashara na Leseni (BRELA).
Uteuzi huu umefanyika kwa kuzingatia wajibu alionao kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali wa Mwaka 1997 Sura 245 kifungu 9(1) kama ilivyorekebishwa Mwaka 2009.
Bi.Loy Waston Mhando anachukua nafasi ya Bw. Emmanuel Kakwezi ambaye
alikuwa anakaimu nafasi hiyo, kabla ya Uteuzi huu Bi.Loy Waston Mhando alikuwa ni Mkurugenzi Idara ya Miliki Ubunifu, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).
Uteuzi huu umeanza rasmi tarehe 19 Novemba, 2019 hadi hapo uteuzi wa kujaza
nafasi hiyo utakapofanyika au itakavyoelekezwa vinginevyo.