Home Mchanganyiko CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI KIBAHA (KFDC) CHAIOMBA SERIKALI KUWAKARABATIA MAJENGO

CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI KIBAHA (KFDC) CHAIOMBA SERIKALI KUWAKARABATIA MAJENGO

0

Mkuu wa chuo cha maendeleo ya wananchi Kibaha (KFDC) Joseph Nchimbi akizungumza na wazazi, wanafunzi na viongozi mbali mbali wa serikali ambao walihudhulia katika mahafali ya kuwaga wanafunzi wa chuo hicho yaliyofanyika mjini Kibaha.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Mjumbe wa bodi wa chuo hicho cha (KFDC)  Elisante Ngure ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za mahafali hayo akisisitiza jambo kwa wanachu wa mwaka wa pili ambao wamehitimu katika fani mbali mbali (PICHA NA VICTOR MASANGU) 

mjumbe wa bodi wa chuo hicho cha (KFDC)  Elisante Ngure ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo wa kulia akiangalia moja ya kazi ya kufua umeme wa majumbani ambayo imefanywa na wanafunzi wa chuoni hapo, hawapo pichani.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

mmoja wa wanafunzi wa Chuo hicho akisoma risala kwa niaba ya wenzake Emmanuel Singambo mbele ya mgeni rasmi  katika sherehe za mahafali hayo ya chuo cha  maendeleo ya wananchi Kibaha Mkoani Pwani .(PICHA NA VICTOR MASANGU).

************************************

VICTOR  MASANGU, KIBAHA.

 CHUO cha maendeleo ya wananchi Kibaha (KFDC) kilichopo Mkoa wa Pwani tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1964 hakijafanyiwa ukarabati wowote katika baadhi ya majengo yake hivyo kupelekea miundombinu  ya madarasa pamoja na  majengo ya utawala kuwa katika hali ya uchakavu hivyo  kuhatarisha usalama wa maisha ya watu hivyo wameiomba serikali ya awamu ya tano kuwasaidia kufanya ukarabati.

Hayo yalisema na Mkuu wa chuo hicho Joseph Nchimbi wakati wa mkutano wa wazazi ambao uliambatana na sherehe za  mahafali pamoja na harambee ya kuchangia ujenzi amebainisha kuwa lengo lao kubwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli ya kuwa na uchumi wa viwanda hivyo wamejipanga kutoa mafunzo zaidi  katika fani mbali mbali kwa vijana ili waweze kujiajiri na kuanzisha viwanda vyao wenyewe.

“Chuo chetu kwa sasa kinafundisha fani mbali mbali ikiwemo ufundi wa umeme wa majumbani, magari,uchomeleaji na uundaji wa vyumba,useremala,ushonaji, ufundi uashi, bomba, kilomo, mifugo, pamoja na fani ya upishi ambazo mafanikio yake ni makubwa kutokana na vijna wengine wamenufaika kupata ajira katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Pwani na Taifa kwa ujumla.

Naye mmoja wa wanafunzi wa Chuo hicho akisoma risala kwa niaba ya wenzake Emmanuel Singambo  alisbainisha kuwepo kwa changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili ikiwemo uchakavu wa vymba vya madarsa,ukosefu wa vitendea kazi,uckakavu mkubwa wa karakana wanazozitumia hivyo wameiomba serikali ya awamu tano kuwasaidia kwa hali na mali lengo ikiwa ni kusoma kwa vitendo  katika mazingira ambayo ni  rafiki.

Kwa upande wake mjumbe wa bodi wa chuo hicho cha (KFDC)  Elisante Ngure ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo amewataka wanafunzi ambao wamehitimu mafunzo hayo kuachana na kuepukana  kabisa na vitendo vya kujiingiza katika uvutaji wa madawa ya kulevya na kushinda vijweni  na badala yake wahakikishe ujuzi walioupata wanautumia kwa maslahi ya nchi hasa katika kuanzisha viwanda vidogo na kujiajiri wao wenyewe.

“Kwa upande wangu mm napenda kuwahasa wanachuo ambao wamehitimu katika chuo hiki cha KFDC kwa sasa inabidi mbadilike achaneni kabisa na mambo ya kukaa vijiweni na kujihusisha na madawa ya kulevya kwani yanapoteza nguvu kazi ya Taifa, hivyo kitu kikubwa elimu ambayo mmeipata itumieni kwa kuleta maendeleo kwa nchi na sio kuitumia vinginevyo,alisema Ngure.

Pia Ngure alisistiza  kuwa katika kuhakikisha kwamba vijana wanajikwamua kiuchumi ni lazima wahakikishe wanaachana na tabia ya kuitegemea serikali pekee katika suala zima la upatikanaji wa ajira na badala yake wanaweze  kujiajiri wao wenyewe  na kuanzisha vikundi mbali mbali kulingana na fani walizozozisome ili kuondokana na wimbi la umasikini

Kwa sasa Chuo cha maendeleo ya wananchi Kibaha ( KFDC) kilichopo Mkoa wa Pwani licha ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katika utoaji wa fani mbali mbali na kuwapa   fursa za ajira katika sekta binafsi na serikalini wanachuo wanaohitimu lakini bado wanahitaji sapoti kubwa ya rasilimali fedha  kutoka serikalini  ili kuweza kutimiza malengo waliyojiwekea.