Wataalam wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, leo
wakiwa eneo la kuwasili abiria maarufu kama “Ukuta wa Tanzania” (Tanzania
Wall) la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere walipofanya ziara
ya mafunzo, ambapo wapo kwenye mkutano wa siku tatu wa kujadili namna ya
kuboresha huduma na miundombinu ya usafiri huo kwa nchi wanachama.
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha (aliyesimama kushoto) akiwasilisha maelezo
yanayohusu majengo matatu ya abiria ya Kiwanja hicho kwa Wataalam wa
Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, leo wameanza mkutano wa
siku tatu wa kujadili namna ya kuboresha huduma na miundombinu ya usafiri
huo kwa nchi wanachama.
Meneja wa Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), Mhandisi Burton Komba (mwenye koti la bluu kushoto), leo akiwaelezea mifumo mbalimbali ya jengo hilo Wataalam wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambao wanashiriki mkutano wa siku tatu wa kujadili namna bora ya kuboresha huduma na miundombinu ya usafiri huo kwa nchi wanachama.
Wataalam wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,
ambao wapo nchini kushiriki mkutano wa siku tatu wa kujadili namna bora ya
kuboresha huduma na miundombinu ya usafiri huo, ambapo leo wametembelea
majengo ya mizigo yaliyopo kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA).
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(aliyenyoosha kidole) akitoa maelezo mbalimbali kwenye ukumbi wa Watu
Mashuhuri (CIP) wa Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja hicho kwa Wataalam wa
Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, waliotembelea leo, ambapo
wapo kwenye mkutano wa siku tatu wa kujadili namna ya kuboresha huduma na
miundombinu ya usafiri huo kwa nchi wanachama.