Baadhi ya wanafunzi Wa kidato cha nne walihitimu wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa viwanda.
Waziri Wa viwanda akitoa vyeti kwa wanafunzi walio Fanya vizuri katika masomo yao.
Baadhi ya wanafunzi Wa darasa la 3 wakiimba kwa ajili ya kuwaaga wahitimu Wa kidato cha nne na darasa la saba.
Mkurugenzi Wa shule za Kaizirege na kemibosi ndg. Yusto Ntagalinda Kaizirege na mke wake pamoja na waziri Wa viwanda.
Wahitimu Wa darasa la saba pamoja na waziri Wa viwanda.
………………….
Na Silvia Mchuruza,Bukoba.
Waziri Wa viwanda na biashara Mh.Innocent Bashungwa amewataka wanafunzi kupewa elimu ya stadi za maisha wakiwa bado shuleni ili kuepukana na adha yoyote ya kujishughulisha pindi wanapokuwa wamemaliza masomo yao ya sekondari.
Ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika maafari ya shule za kaizirege na kemibosi mkoani kagera katika manispaa ya bukoba ambapo amewataka walimu kuwapa mafunzo hata ya stadi mbali mbali ikiwemo hata useremala kipindi wakiwa shuleni ili kupata ujuzi Wa ziada.
Hata hivyo amewapongeza wanafunzi hao kutokana na kuwa na matokeo mazuri katika mitihani yao ya kitaifa ambapo katika mtihani Wa darasa la saba mwaka huu imekuwa ya kwanza kiwilaya na ya kumi kitaifa na kuufanya mkoa kuwa Wa nne kitaifa.
“Nimejua siri kubwa ya shule hizi kwanza ni kutokana na kuwa na maeneo mazuri ya kusomea lakini pia wanafunzi nao wamefundishwa kujituma ndiyo maana wanafanya vizuri na ndiyo maana wana mafanikio mazuri miaka 13 ya shule hizi toka kuanza kwakweli tumeona mafanikio take”
Nae Mkurugenzi Wa shule hizo Ndg.Yusto Ntagalinda Kaizirege ametoa shukrani kubwa kwa wazazi katika kuhakikisha wanawafanya watoto wao wanapata elimu bola katika ufundishwaji huku akiongeza kuwa shule hizo zina mda Wa miaka 13 toka kuanzishwa kwake na hii ikiwa ni mahafari ya kumi kufanyika shuleni hapo.