Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi ameongoza sherehe za mahafali ya 11 kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom ‘ Kom Secondary’ iliyopo katika eneo la Butengwa katika manispaa ya Shinyanga ambapo jumla ya wanafunzi 189 kati yao wasichana 80 wavulana 109 wamehitimu elimu ya kidato cha nne katika shule hiyo.
Mahafali hayo yamefanyika leo Jumamosi Novemba 16,2019 katika viwanja vya shule hiyo na kuhudhuriwa na mamia ya wazazi,wageni waalikwa,wanafunzi na watu mbalimbali wenye mapenzi mema.
Akizungumza wakati wa Mahafali,Mgeni rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawalipia ada watoto wao kwa wakati.
“Nimeambiwa kuna baadhi ya wazazi wanachelewa kulipa ada.Niwakumbushe tu kuwa ukimpeleka mtoto katika shule binafsi maana yake una uwezo wa kulipa ada, sasa lipeni. Elimu ni gharama, hata kwenye shule za serikali ‘ Public Schools’ kuna gharama,kuna nguvu za wananchi”,alisema Kahundi.
“Ni muhimu kumpeleka shule mtoto mara tu shule inapofunguliwa,kwani shule ikifunguliwa masomo yanaanza. Usimuweke mtoto nyumbani,anafanya nini nyumbani muda wa shule?,alihoji Kahundi.
Afisa Elimu huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi kuwakatia bima ya afya watoto wao ili kurahisisha matibabu pindi wanapougua.
“Vijana mnarudi nyumbani mnatakiwa kuwa watii kwa wazazi wenu,nanyi wazazi msijaribu kuwaozesha wanafunzi hawa waliohitimu kidato cha nne.Msiende kuozesha watoto hawa”,alisema Kahundi.
Kahundi aliipongeza shule ya Kom kwa mwenendo mzuri kitaaluma na kinidhamu kwani imeendelea kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali ngazi na mkoa na taifa.
Awali Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom, Jackton Koyi alisema shule hiyo imeendelea kufanya vizuri kitaaluma ambapo katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 wanafunzi 179 walihitimu kati yao 167 walijiunga na kidato cha tano.
Aidha kwa kipindi cha miaka 10 kati ya mwaka 2009 hadi 2018,Koyi alisema jumla ya wanafunzi 1420 wamehitimu kidato cha nne kati yao wanafunzi 1093 walichaguliwa kuendelea na kidato cha tano.
Alisema wanafunzi waliobaki 327 wengi wao wamejiunga na vyuo mbalimbali vikiwemo vya uhasibu,biashara,ualimu,uuguzi,sheria n.k huku akibainisha kuwa mafanikio hayo yanatokana na kazi nzuri inayofanywa na walimu darasani pamoja na nidhamu ya hali ya juu ya wanafunzi.
Akisoma taarifa ya shule,Mkuu wa Shule ya Sekondari Kom, Mwita Waryoba alisema shule hiyo iliyosajiliwa mwaka 2006 ikiongozwa na kauli mbiu ‘ Elimu bora kwa wote – Quality Education for All’,alisema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 579 kati yao wavulana ni 314 na wasichana 265 huku walimu wakiwa ni 32 hivyo uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi ni 1:18.
Alizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo ni pamoja na gharama kubwa za uendeshaji zinazosababishwa na mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha,baadhi ya wazazi kutolipa ada kwa wakati hivyo kuwafanya watoto wachelewe kufika shule inapofunguliwa na baadhi ya watoto kutowalipia watoto wao bima ya afya.
Mbali na shule ya sekondari Kom,pia kuna shule ya awali na shule ya msingi Kom iliyoanzishwa mwaka 2016 ipo nyuma ya ofisi za KASHWASA umbali wa takribani mita 500 kutoka shule ya sekondari Kom. Hali kadhalika wameanzisha kituo cha watahiniwa wa kujitegemea wa kidato cha nne na wale wa QT ‘Private candidates & Qualifying test”.
Mgeni Rasmi wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom,Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akikata utepe kwenye mahafali hayo.Aliyevaa nguo nyeusi nyuma ni Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom, Jackton Koyi. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mgeni Rasmi wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom,Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akiwasalimia wazazi na wageni waalikwa kwa kuwapungia mkono.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakiwa katika maandamano kuingia ukumbini wakati wa sherehe za mahafali ya 11 kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom ‘ Kom Secondary’ iliyopo katika eneo la Butengwa katika manispaa ya Shinyanga. Jumla ya wanafunzi 189 wamehitimu elimu ya kidato cha nne katika shule hiyo.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakiwa katika maandamano kuingia ukumbini.
Mgeni Rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akizungumza wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom, ambapo alitumia fursa hiyo kuipongeza shule ya Sekondari Kom kwa mwenendo mzuri kitaaluma kwani imekuwa ikifanya vizuri kwenye mitihani mbalimbali.
Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom, Jackton Koyi akitoa neno la salamu wakati wa Mahafali ya 11 kidato cha nne shule ya Sekondari Kom.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kom, Mwita Waryoba akisoma historia ya shule ya Sekondari Kom. Warioba aliwaomba wazazi kuwaongoza na kuwaelekeza vizuri vijana waliomaliza elimu ya kidato cha nne wakati wakisubiri matokeo yao yatakayowawezesha kuendelea na masomo yao ya kidato cha tano na vyuo.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakikata keki maalumu wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakikabidhi zawadi ya keki kwa walimu wa shule ya sekondari Kom.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wageni waalikwa wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Onesho la mitindo ya ubunifu wa mavazi likiendelea.. Pichani ni vijana wakionesha ubunifu wa mavazi ya Mama Afrika wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom.
Onesho la vazi mavazi ya wahudumu wa kwenye Ndege likiendelea wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom.
Vijana wa Skauti wakionesha michezo ya ukakamavu wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne Kom Sekondari mwaka 2019.
Mgeni Rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akizungumza wakati wa Harambee kufanikisha ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari Kom,ambapo makadirio ya gharama ya ununuzi wa vifaa hivyo ni milioni 6.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akichangia pesa wakati wa Harambee kufanikisha ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari Kom.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akimpa Kampani ya kucheza mzee aliyejitokeza kuchangia pesa huku akicheza muziki wakati wa Harambee kufanikisha ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari Kom.
Ukawadia muda wa kugawa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne 2019 katika shule ya Sekondari Kom.
Zoezi la kugawa vyeti vya kuhitimu kidato cha nne likiendelea.
Zoezi la kugawa vyeti vya kuhitimu kidato cha nne likiendelea.
Walimu wa shule ya sekondari Kom wakikabidhi zawadi kwa Mgeni rasmi ,Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi.
Mshereheshaji ‘MC’ wakati wa mahafali akiendelea kutoa utaratibu wakati wa mahafali hayo.
Wazazi wakifurahia na kijana wao.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog