Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Bi.Esther Mwakilima,akizungumza wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa Viongozi ,Wafanyakazi na Wananchama wa kazi Saccos Limited uliofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti Kazi Saccos LTD,Omari Sama,akitoa taarifa kwenye Mkutano Mkuu wa Viongozi ,Wafanyakazi na Wananchama wa kazi Saccos Limited uliofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kikao Bi.Venerose Mtenga,akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Viongozi ,Wafanyakazi na Wananchama wa kazi Saccos Limited uliofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Bi.Esther Mwakilima,akielezea jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Viongozi ,Wafanyakazi na Wananchama wa kazi Saccos Limited uliofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Bi.Esther Mwakilima,akipongezwa na Mwenyekiti wa Kikao Bi.Venerose Mtenga, mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Viongozi ,Wafanyakazi na Wananchama wa kazi Saccos Limited uliofanyika jijini Dodoma.
Afisa Sheria Mwandamizi mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi (WCF) Bw.Deo Victor,akitoa maada katika mafunzo na Mkutano Mkuu wa Viongozi,Wafanyakazi na Wanachama wa kazi Saccos Limited uliofanyika leo jijini Dodoma.
Mratibu kutoka TACAIDS Mkoa wa Dodoma ,Eriko Kawanga,akitoa taarifa kwenye mafunzo na Mkutano Mkuu wa Viongozi,Wafanyakazi na Wanachama wa kazi Saccos Limited uliofanyika leo jijini Dodoma.
Kamishna wa Kinga na Tiba kutoka Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya Dkt.Peter Mfisi,akitoa maada kuhusiana na madawa ya kulevya kwa wadau waliohudhuria Mafunzo na Mkutano Mkuu wa Viongozi,Wafanyakazi na Wanachama wa kazi Saccos Limited uliofanyika leo jijini Dodoma.
Afisa Ushirika Jiji la Dodoma Bw.Massawe Grayson,akizungumzia kuhusu Saccos Limitde wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Viongozi ,Wafanyakazi na Wananchama wa kazi Saccos Limited uliofanyika jijini Dodoma.
Mkaguzi wa Ushirika wa Mkoa wa Dodoma,Dorah Meta,akisoma taarifa ya ukaguzi ya mwaka 2018 wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Viongozi ,Wafanyakazi na Wananchama wa kazi Saccos Limited uliofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Bi.Esther Mwakilima,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Viongozi ,Wafanyakazi na Wananchama wa kazi Saccos Limited uliofanyika jijini Dodoma.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
……………………..
Na Alex Sonna, Dodoma
WANACHAMA wa Kazi Saccos Limited wasiorejesha mikopo wapo kikaangoni kufikishwa mahakamani ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria kutokana na kukiuka mikataba yao.
Agizo hilo limetolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu, Esther Mwakilima akifungua mkutano mkuu wa Saccos hiyo, uliofanyika jijini Dodoma.
Amesema kuna wanachama ambao wamekuwa na mwenendo mbaya wa kukopa bila ya kutaka kurejesha kwa wakati na kwa makusudi.
“Naomba niseme wazi kuwa suala hili lipo mezani kwangu na nimeshatoa maelekezo ya awali kwa Mwenyekiti wenu kuwa wale wote ambao hawataki kurejesha mikopo hiyo kama mlivyokubaliana kwenye mikataba yenu, wachukuliwe hatua stahiki za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani,”amesema.
Mwakilima uongozi wa Saccos hiyo umeazimia kuwafikisha watumishi hao mahakamani mara baada ya Mkutano huo.
“Ofisi yangu ilishatoa maelekezo kwa watumishi waliopo Ofisi ya Waziri Mkuu(KVAU) kuhakikisha wanakopa kwa busara na kulipa madeni yao kwa wakati,Hatutasita kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa yeyote atakayepatikana na hatia na kuhukumiwa kwa tuhuma za namna hii,”amesema.
Kaimu Katibu huyo amewataka kubadilika kuanzia sasa kila mmoja awajibike kwa chama kwa kukijali, kukithamini na kuheshimu.
Amewaasa kuweka akina, kukopa na kurejesha kwa wakati ili wapate manufaa zaidi ya wanayopata kwasasa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Saccos hiyo, Omari Sama amesema fedha zilizopo kwenye mzunguko wa wanachama ni takribani Sh.Milioni 200.
“Changamoto kubwa tuliyonayo ni madeni mabaya kwa wanachama ambao wengine wapo kwenye Mawizara mbalimbali na chama chetu kina watumishi wa kada zote, kuna Wakurugenzi wapo kwenye Wizara zingine tunawadai na hawajalipa kwa kipindi kirefu,”amesema.
Amesema madeni hayo yapo kwenye hoja za wakaguzi na wamekuwa wakikaguliwa na Shirika la COASCO kila mwaka.
Ametaja changamoto nyingine ni suala la ofisi kwa kuwa wanalipa pango na inaonesha watapata hasara kutokana na gharama kubwa za uendeshaji na mikopo isiyolipika.
“Hawa wanaodaiwa wa kuanzia mwaka 2015 hadi sasa taarifa zao zipo watapelekwa mahakamani, hawa wa nyuma taarifa zao bado ngumu lakini tunaendelea kuwafuatilia ili waweze kulipa,”amesema.