Na.Majid Abdulkarim
Timu ya Mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI Queens) imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali katika Ligi ya Muungano Zanzibar 2019.
TAMISEMI Queens wamefuzi hatua ya nusu fainali wakiwa na arama nane baada ya kucheza mechi nne na kushinda zote wakisalia na mchezo mmoja wa kukamilisha ratiba watakao cheza na timu ya Eagle ya Dar es salaam.
Akizungumza baada ya mchezo wa leo Mwalimu wa Timu ya TAMISEMI Queens Maimuna Rajabu Kitete baada ya ushindi wa mechi ya leo kati yao na timu ya Zimamoto ya Zanzibar mchezo uliyofanyika huko visiwani Zanzibari na TAMISEMI Queens kuibuka na ushindi wa gori 47 kwa 36 dhidi ya Zimamoto.
“Nimejipanga vizuri na wachezaji wako vizuri kufanya vyema katika hatua hii ya nusu fainali ili kuhakikisha tunatwaa ubingwa katika michuano hii ya Ligi ya Muungano Zanzibar 2019 japo ni mara yetu ya kwanza kushiriki michuano hii naimani tutafanya vizuri . ameeleza Mwalimu Kitete
TAMISEMI Queens ni timu iliyomo katika kundi B ikiwa na timu za JKT Mbweni, Mafunzo ya Zanzibar, Eangle ya Dar es salaam, Makotopola ya Dodoma na Zimamoto ya Zanzibar.
TAMISEMI Queens kati ya Mafunzo waliibuka na ushindi wa gori 49 kwa 45, TAMISEMI Queens kati ya JKT Makotopola walipata ushindi wa gori 37 kwa 34, TAMISEMI Queens kati ya JKT Mbweni walishinda gori 54 kwa 50 na ushindi uliyowapeleka hatua ya nusu fainali ni wa gori 47 kwa 36 kutoka kwa Zimamoto ya Zanzibar.