Sehemu ya wahitimu wa chuo cha VETA Mikumi wakifurahi wakati wakiingia katika viwanja vya Mahafali katika Chuo hicho
Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare akipata maelezo kutoka mwanafunzi wa ngazi ya tatu katika ya uunganishaji Stanford Ngozo namna walivyotengeneza kabati wakati mkuu wa mkuu huyo alipotembelea karakana hiyo, mahafali ya 22 ya Chuo cha VETA Mikumi Mkoani Morogoro.
Picha ya pamoja na wahitimu waliopata tuzo mbalimbaliKaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Mikumi Emmanuel Munuo akizungumza kuhusiana na historia ya chuo hicho na mafanikio waliyoyapata katika kuandaa vijana wenye ujuzi .
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Adam Mgoi akizungumza kuhusiana na faida ya Chuo hicho kwa wakazi wa Kilosa kupata stadi za ufundi wakati wa Mahafali ya Chuo cha VETA Mikumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
*************************************
Na Chalila Kibuda,Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare ameahidi kuwa Balozi wakusaidia wahitimu wa Chuo cha VETA Mikumi kwa wale wataokafanya vizuri kwenye masomo yao baaada yakumaliza mitihani yao kwa mwaka huu
Kauli hiyo Ameitoa wakati wa mahafali ya 22 ya chuo cha ufundi stadi mikumi mkoani morogoro nakueleza kuwa mkoa wa morogoro unayo miradi mikubwa inayotekelezwa kama ule mradi wa kufua umeme wa bwawa la mwl nyerere ambao unahitaji watalaamu wanaozalishwa kutoka vyuo vya ndani na hivyo yeye akiwa kiongozi atahakikisha watakaofaulu vizuri wanapata ajira kwenye miradi hiyo
Mkuu huyo wa mkoa ameeleza kuwa serikali ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kuwaendeleza vijana kwakutoa wataalumu ambao wanatoka kwenye vyuo mbalimbali ikiwemo Veta na hivyo kila mwanafunzi anayesoma veta anatakiwa kufahamu kuwa ipo miradi inayowahitaji wao kuitumikia ikiwemo kujiajiri mwenyewe pamoja na kupenda kazi,kutafyta fursa,kuwa wajasiliamali, na kujiendeleza kitaaluma ili kumudu mabadiliko ya sayansi na teknolojia
Nae kaimu mkuu wa chuo Veta Mikumu Emmanuel Munuo ameziomba asasi zisizo za serikali na wadau kuifaga mfano wa shirika la plan international kwa kutafyta vijana walioko vijijini kutambua mahitaji yao na kasha kuwapatia mafunzo ya ufundi stadi na elimy ya ujasiliamali ili kuwatengenezea fursa za kujiajiri au kuajiriwa katika sekta rasmi na isiyo rasmi.
Nao baadhi ya wazazi na walezi wamewataka vijana wanaohitimu masomo kuwa waadilifu nakuutumia ujuzi waliupata kwa manufaa kwa jamii na taifa pamoja nakusoma kwa bidiii ili kuitumia fursa yakauli ya mkuu wa mkoa yakutumia miradi iliyopo Morogoro kwakupata ajira
Jumla ya wahitimu 240,Wavulana 176 na Wasichana 64 wanahitimu kwa fani mbalimbali chuoni hapo.