Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt Emmanuel S. Shindika katikati mwenye suti ya kijivu wakati akifunguarasmi kikao cha Baraza la Wafanyakazi linaloendelea katika ukumbi wa VETA Dodoma
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt Emmanuel S. Shindika mwenye suti ya kijivu katikati akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Chuo cha Utumishi wakimsiliza
Mwenyekiti wa Baraza
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Chuo cha Utumishi wa Umma wakifuatilia Mkutano
…………………
Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Dkt.Emmanuel Selemani Shindika amewataka watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu.
Dkt Shindika ameyasema hayo Jjini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa VETA Dodoma.
Alisema Chuo cha Utumishi wa Umma kimebeba majukumu ya kuhakikisha kuwa mafunzo yenye ubora yanatolewa kwa watumishi wa umma. Katika kutoa mafunzo hayo ni lazima kuonesha ushirikiano, umoja, mshikamano, ufanisi na uadilifu mkubwa kwa kuzingatia sheria, kanuni,taratibu na miongozo mbalimbali ya Chuo.
Alisema uzoefu unaonesha kwamba vikao vya Baraza la Wafanyakazi vimekuwa na faida mkubwa mahala pa kazi. Kwa kupitia Baraza la Wafanyakazi Chuo kimefanikiwa kuongeza ufanisi na mshikamano mkubwa kati ya Watumishi na Menejimenti pamoja na wadau wetu” alisema Dkt Shindika.
Hata hivyo Afisa Mtendaji Mkuu huyo amesema Taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazoikabili kwa muda mrefu ikiwemo ya uhaba wa majengo kwa ajili ya madarasa, na akasema kwamba juhudi mbalmbali ili kutatua changamoto hiyo.