Wafanyabiashara ya samaki Wilayani Nyasa,wakiwa katika soko jipya la fisheries ambalo mkuu wa wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba, aliipa halmashauri ya Wilaya ya Nyasa siku saba kuanzisha soko la samaki ili kutatua changamoto iliyokuwa inawakabili wafanyabiashara ya samaki Wilayani Nyasa, ya kutokuwa na eneo maalumu ya kuuzia samaki.(picha na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa)
…………………..
Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa imetekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Bi Isabela Chilumba la kuanzisha Soko la samaki katika eneo la Fisheries Wilayani hapa, kwa kipindi cha siku saba.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa alitoa agizo hilo octoba 30 mwaka huu, wakati akiongea na wavuvi,p amoja na wachuuzi wa mazao ya uvuvi kwa lengo la kutatua changamoto ya kutokuwa na Soko la samaki wilayani Nyasa.
Uchunguzi uliofanyika na mwandishi wa habari hizi umebaini kabla ya kutimia siku saba za agizo hilo, soko la samaki lilikuwa limeshaanza katika jengo la karakana ya kutengenezea boti, ambalo lilikuwa halitumiki. wavuvi wengi wa Mbamba-bay wamefurahia uwepo wa soko hili ambalo limetatua changamoto, kero ya kutokuwa na sehemu maalumu ya kuuzia samaki, iliyokuwa inawakabili wavuvi na wachuuzi wa samaki.
Mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi Wilaya ya Nyasa Bernard Semwaiko amethibitisha kuanza kwa soko hilo la samaki Mjini Mbamba-bay na leo amefanya kikao na uongozi wa kamati ya soko la samaki Mbamba-bay kwa lengo la kutatua changamoto zingine katika soko hilo la samaki.
Wafanyabiashara wa samaki wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba, na Uongozi wa Halmashauri Nyasa kwa kuanzisha Soko la Samaki , na kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanatekeleza majukumu yao bila kikwazo chochote.