Home Mchanganyiko Wafanyakazi wa EATV  watembelea kiwanda cha TBL Dar

Wafanyakazi wa EATV  watembelea kiwanda cha TBL Dar

0

Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TBL,akiwaeleza wafanyakazi wa EATV shughuli za kiwanda

Mtaalamu wa upishi wa biawa TBL,Elicana Ng’osha akiwapatia maelezo kwa wafanyakazi wa EATV

******************************

Baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha luninga cha EATV, wamefanya ziara katika kiwanda cha bia cha TBL kilichopo jijini Dar es Salaam, na kuweza kujionea shughuli za uzalishaji sambamba na kuelezwa jinsi kampuni hiyo ilivyojipanga kuhakikisha inakwenda sambamba na agenda ya serikali ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Katika ziara hiyo, walipata, alipata maelezo ya jinsi kampuni ya TBL Group chini ya kampuni mama ya kimataifa ya ABInBEV, inavyoendesha biashara zake sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali katika kufanikisha Malengo Endelevu ya Dunia (SDGS’s).

Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TBL, Amanda Walter, aliueleza ujumbe uliojumuisha waandishi wa habari wa kituo hicho, jitihada zinazofanywa na kampuni kutekeleza masuala hayo kwa lengo lakuifanya jamii kuwa na maisha bora na endelevu  katika maeneo ya kusaidia miradi ya maji salama, kuhamasisha matumizi mazuri ya maji, utunzaji wa mazingira, kuwezesha wanawake kiuchumi, kutoa elimu ya ujasiriamali sambamba na  elimu ya unywaji wa kistaarabu, kuwezesha wakulima wadogo wanaoiuzia kampuni malighafi na kutoa ajira nyingi kwa wananchi wa Tanzania kupitia mtandao wa biashara zake.

Amanda, pia alieleza kuwa TBL imekuwa  mstari wa mbele kuchangia pato la serikali kwa njia ya kulipa kodi ambapo imeweza kutunukiwa tuzo ya Mlipa Kodi Bora nchini na tuzo nyinginezo baadhi yake zikiwa tuzo ya Rais ya Mzalishaji Bora na tuzo ya Mwajiri bora.