******************************
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Serikali imewataka vijana kuanza kubadilisha fikra kwa kuangalia zaidi shughuli wazifanyazo kwa kina na tija ili kuwezesha kupata msingi wa biashara kwa kuzisimamia ipasavyo fursa mbali mbali za kukuwa kiuchumi.
Kwa Muktadha huo serikali inatambua vijana ni kundi kubwa linalofanya nguvu kazi ya Taifa ambayo ni sawa na asilimia 56 ya nguvu kazi yote,Hata hivyo vijana ndiyo wameathiriwa sana na changamoto ya ukosefu wa ajira ukilinganisha na makundi mengine,Nikirejea Utafiti wa Nguvukazi wa mwaka 2014 ambao unaonesha wazi kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana nchini ni asilimia 11.7, kiwango hiki ni zaidi ya kiwango cha jumla cha ukosefu wa ajira kwa Taifa (asilimia 10.3). Changamoto hii inaifanya Serikali yetu chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuweka mikakati endelevu ya kuliwezesha kundi la vijana kupata ujuzi stahiki wa kujiajiri na kushiriki ipasavyo katika shughuli za kiuchumi na ujenzi wa Taifa.
Hayo yameelezwa na Naibu waziri wa Kazi ajira na watu wenye Ulemavu Anthony Mavunde akifunga mafunzo siku 8 ya Ujasiriamali na usimamizi wa biashara yaliondaliwa na Tume ya Taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ofisi ya waziri mkuu jijini Arusha.
Alisema kuwa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa Vijana Wafanyabiashara ni sehemu ya Programu ya Taifa ya Ukuzaji,Ujuzi inayotekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu-KVAU kwa kushirikiana na Wadau. Aidha mpangu huo wa Taifa wa Ukuzaji Ujuzi ni moja ya mikakati muhimu ya Serikali ya awamu ya tano kuiwezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi stahiki wa kujiajiri.
Alisema kuwa lengo la mafunzo haya ni kubadilisha mitazamo ya vijana katika kuchangamkia fursa mbali mbali za kiuchumi ndio maana mwitikio wa Vijana wa Mkoa wa Arusha kushiriki mafunzo ni mkubwa sana na wametoka katika Halmashauri nne za Mkoa wa Arusha. Hali hii inadhihirisha umuhimu wa programu hii kwa vijana wajasiriamali ambayo itawasaidia kukuza na kuendeleza biashara zao, kukuza kipato na kuboresha maisha yao. Hali kadhalika,
“Katika Mikoa yote nane ambako mafunzo yamefanyika, vijana wameonesha uhitaji mkubwa wa kupatiwa mafunzo haya. Hali hii inaashiria kuwa kuna kila sababu ya kuendeleleza mafunzo haya katika mikoa yote ya Tanzania ili kuwapatia vijana nyenzo muhimu za kuwawezesha kufanya biashara kwa mafanikio na tija. Vijana wa Mkoa wa Arusha mliobahatika kupata mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa biashara, nawaasa kuwa tumieni ujuzi mliopata katika mafunzo haya kuendeleza na kuboresha biashara zenu”alisema.
“Mikopo haina maana sana kama hauna elimu kwa kuwa tumeona vijana wengi wakishindwa kurudisha fedha za mikopo kwa kukosa elimu ikiwemo mikopo ya asilimia 10 ndio maana tumeona tuwasaidie kupata elimu kuwezesha kutumia mikopo na mitaji kukuza biashara zenu”alisema Mavunde.
Alitanabaisha kuwa matarajio ya serikali ni kuongeza ajira za moja kwa moja ikiwemo pia makampuni kwa kuimarisha shughuli za vijana kote nchini kwa kuwapatia mafunzo ya kuwawezesha kiuchumi na mafunzo ya aina hii tutayafanya nchi nzima ila tumeanzia kwenye mikoa nane na jumla ya vijana 46,000 watafikiwa na mafunzo hayo kupitia mipango mbalimbali ya
Awali Meneja ufuatiliaji na Uratibu miradi wa tume ya taifa uwezeshaji wananchi Kiuchumi Flora Kajela Alisema kuwa Mkoa wa Arusha ni Mkoa wa nane katika utekelezaji wa mpango huo ambayo imetekelezwa katika mikoa nane ya Tanzania Bara. Mikoa 18 iliyobaki ambayo haijashiriki kwenye awamu hii ya mafunzo itashiriki katika awamu ya pili kulingana na upatikanaji wa fedha na hivyo kuwezesha kuwafikia jumla ya vijana 4,000 hapa nchini.
Alieleza kuwa Mikoa nane iliyoshiriki katika awamu hii ya mafunzo ikiwemo Arusha, imechaguliwa miongoni mwa mikoa yenye wajasiriamali wengi vijana ambao walitamani sana kuwa sehemu ya shughuli hii. Hivyo, ni vema vijana wa Arusha mkaitumia nafasi hii vizuri kwa kuhakikisha kuwa mnatumia stadi mlizozipata kwenye mafunzo haya ili muweze kupata tija katika shughuli zenu mnazozifanya.
Alisema mafunzo hayo yalijikitazaidi juu ya upatikanaji wa mitaji,masoko ya bidhaa,uongezaji bidhaa thamani program za kuongezea ujuzi na stadi za kazi kwa lengo la kuboresha shughuli za vijana hao kwenye uchumi, ambapo Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi limekuwa likifanya Mafunzo ya aina hii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa maendeleo, taasisi za umma, sekta binafsi na jamii kwa ujumla,Mafunzo yamekuwa yakitolewa kwa njia mbalimbali ili kuwapatia vijana stadi ambazo zinahitajika katika soko la ajira na bidhaa.
Kwa upande wake Katibu tawala mkoani hapa Richard Kwitega alisema mkoa huo umefanikiwa katika shughuli za kuwezesha wananchi kiuchumi ikiwemo kutoa mikopo ya bodaboda kwa vijana zaidi ya 200 na kinamama ntilie 100 ambapo kwenye fedha za halmashauri zaidi ya billion 2.412 zilitolewa kwa vijana mkoani hapa kwa miaka ya 207\18.nawajulisha washiriki kuwa kila Mkoa una fursa ambazo zinaweza kutumiwa na wajasiriamali ili kujiendeleza kiuchumi.
Alisema kuwa mkoa kwa sasa upo kwenye mpango wa kuandaa vijana kwenye mafunzo ya mpango wa kitaifa wa mafunzo ya kuwesha vijana ya Kitalu nyumba,ambapo ni imani ya mkoa wote yale vijana waliofundishwa yataleta tija kwenu na taifa kwa ujumla na kuboresha shughuli za kiuchumi.