Prof. Lazaro S.P. Busagala,Mkurugenzi Mkuu (TAEC) wa kwanza kulia aliyenyoosha mkono

Mkurugenzi Mkuu Prof. Lazaro Busagala wa pili kutoka kulia akishuhudia maendeleo ya awali ya ujenzi wa maabara awamu ya pili

 Clay Semmy Moshi, Kulia  Injinia msaidizi kwa upande wa Mkandarasi akitoa maelezo ya kitaalam kwa Mkurugenzi Mkuu kuhusiana na mradi

……………………………………………………

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ( TAEC), Prof. Lazaro Busagala amekagua hatua za awali za maendeleo ya mradi wa ujenzi wa maabara ya awamu ya pili ulioanza hivi karibuni katika Kiwanja Na. 216 Block J, Njiro, Jijini Arusha

Ujenzi huu wa mradi umeanza rasmi tarehe 19/09/2019 na unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu endapo hakutatokea na changamoto yoyote

Jumla ya shs Bilioni 10,447,749,433.24 zinatarijiwa kukamilisha mradi huu mkubwa, na mara mradi utakapokamilika takribani ya watanzania wasiopungua 200 watapata ajira

Hizi ni juhudi zingine za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wetu mpendwa Mhe. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha mionzi haileti athari kwa Watanzania, Mazingira, Wafanyakazi na Wagonjwa

Imetolewa na

Peter G. Ngamilo

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania