Wakazi wa kijiji cha Itamba kata ya Mdandu wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe wamelazimika kuunganisha nguvu zao kwa kushirikiana mpango TASAF unaofadhiliwa na shirika la OPEC kung’oa visiki pamoja na kuchonga barabara tano zenye jumla ya urefu wa km 7.3 kuelekea maeneo ya kilimo cha vitunguu,nyanya,Viazi na Hoho wilayani humo ili kuepukana na adha ya kukatika kwa mawasiliano msimu wa masika na kuathiri shughuli za usafirishaji wa mazao kwenda sokoni.
Wakieleza nia ya kufanikisha ujenzi wa barabara hiyo wakazi hao wamesema ni kutokana na kusimama kwa shughuli za mawasiliano na uchukuzi ambao umekuwa ukijitokeza kila mwaka nyakati za masika kutokana na ubovu mkubwa na kusababisha magali ya mizigo kushindwa kufika maeneo ya uzalishaji na kisha kuacha mazao yakiozea shambani.
Aidha wakazi hao ambao ni wanufaika wa TASAF wanasema nyakati ambazo barabara haipitiki husababisha bei za mazao kupanda bei na kudai kwamba kitendo cha mpango huo kuamua kushirikiana nao kuzitatua ukiwemo mradi wa uchongaji wa barabara hiyo utaleta matokeo chanya kiuchumi kwa wakazi wa kata ya mdandu,Kidugala na nyingine za jirani ambazo zinategemea barabara hiyo kusafirisha mazao
Kata ya Mdandu imekuwa ikiendelea kukabiliwa na changamoto lukuki katika sekta ya elimu,afya,maji na barabara lakini kwanini kijiji kiliamua kupeleka maombi maalumu serikali kupitia mradi wa TASAF ili kusaidiwa ujenzi kwa asilima 90 huku wakiacha changamoto nyingine kubwa na kuahidi kuchangia asilimia 10 kufanikisha mradi huo wa barabara.Huyu hapa diwani wakata ya Mdandu Anaupendo Gombela anafafanua.
Nae afisa ufatiliaji wa miradi ya TASAF katika wilaya za Mbarali,Wanging’ombe na Ludewa Edwin Mlowe katika utekelezaji wa mradi huo wa km 7.2 uliogharimu mil 72 umefanikiwa pia kutoa ajira za muda kwa wanufaika wa mpango hatua ambayo ilizidi kuwaongezea kipato na kuahidi kuendelea kushirikiana na wananchi kutatua kero zinazowakabili.
Katika mkoa mzima wa Njombe TASAF imetekeleza miradi yenye thamani ya zaidi ya bil 13 katika awamu ya kwanza yenye miaka mitano.