***********************************
EMMANUEL MBATILO
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeandaa mbio zijulikanazo kama UDSM Half Marathon ambazo zitafanyika siku ya Jumamosi Desemba 7 mwaka huu kwa lengo la uchangishaji kwaajili ya ya kituo cha wanafunzi.
Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam, Rais wa UDSM half Marathon,Balozi Mwanaidi Maajar amesema kuwa kila mmoja kwa ushiriki wake atakuwa ameshiriki kwenye malengo yaliyoelezwa, Km 21.1, Km10 na Km5.Kila atakayefanikiwa kumaliza mbio, katika hizo ruti tatu atapata medali ya ushindi.
“Kutakuwa na zawadi kwa washindi watano wa kwanza wa kike na wakiume katika Km21 na Km 10. Pia kutakuwa na zawadi za washindi wawili wa mwanzo kwa kundi la walemavu”.Amesema Balozi Mwanaidi.