Mratibu wa Lishe-OR Tamisemi_Dodoma, Dokta.Mwita Waibe akiwasilisha mada katika semina ya Masuala ya Lishe kwa wanahabari iliyofanyka leo jijini Dar es Salaam kwa lengo la ufikishaji taarifa kwa wananchi kuhusu masuala ya lishe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Agri Thamani Foundation Bi.Neema Lugangira akizungumza na wadau mbalimbali wa habari katika semina ya Masuala ya Lishe kwa wanahabari iliyofanyka leo jijini Dar es Salaam kwa lengo la ufikishaji taarifa kwa wananchi kuhusu masuala ya lishe.
Baadhi ya wamahabari wakitoa maoni yao katika semina ya Masuala ya Lishe kwa wanahabari iliyofanyka leo jijini Dar es Salaam kwa lengo la ufikishaji taarifa kwa wananchi kuhusu masuala ya lishe.
Wadau mbalimbali wa habari wakipata picha ya pamoja semina ya Masuala ya Lishe kwa wanahabari iliyofanyka leo jijini Dar es Salaam kwa lengo la ufikishaji taarifa kwa wananchi kuhusu masuala ya lishe.
***********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Wazazi na Walezi wametakiwa kuhakikisha lishe inapatikana kwa mama kwa zile siku 1000 toka mimba inatunga hadi mtoto anapokuwa na umri wa miaka 2 kwani ni muhimu kwa makuzi ya akili na mwili.
Ameyasema hayo leo Mratibu wa Lishe-OR Tamisemi_Dodoma, Dokta.Mwita Waibe katika Semina kwa Wanahabari kuhusu elimu ya Lishe iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika semina hiyo,Dkt.Waibe amesema kuwa uchumi utaendelea kuathiriwa kama hatutawekeza kwenye suala la lishe kwani fedha zote ambazo zinatumika kwa watu ambao wameathirika kwa kutopata lishe zingeweza kutumika kuleta maendeleo mengine hapa nchini.
“Serikali tumekuwa tukiwaita wadau mbalimbali wa lishe kuongea nao ili elimu iweze kuwafikia wananchi wengi hasa wa vijijini kwamba suala la lishe ni suala muhimu sana la kuangalia”. Amesema Dkt.Waibe.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Agri Thamani Foundation Bi.Neema Lugangira amewataka wanahabari kuhakikisha wanasaidia kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya lishe ili kuepukana na matatizo ya udumavu hapa nchini.