Home Mchanganyiko VSO YATUA KAGERA KWA AJILI YA WATU WENYE ULEMAVU NA MAKUNDI MAALUMU.

VSO YATUA KAGERA KWA AJILI YA WATU WENYE ULEMAVU NA MAKUNDI MAALUMU.

0

********************************

Na Silvia Mchuruza.
Bukoba.

Shirika la huduma za kujitolea VSO kutoka Dar es salaam limetoa mafunzo na ujuzi kwa wadau na watu wenye ulemavu jinsi ya kuwapa kipaumbele katika jamii mkoani kagera.

Akizungumza Afisa mradi Bi Juliet Mgasa wakati akiwasirisha taarifa ya shirika la VSO amesema kuwa shirika hilo limefanya utafiti miaka miwili nchini ambapo lilianza kufanza kazi mwaka 1960 na pia limejikita katika kufuatilia elimu jumuishi hasa kwa watu wenye ulemavu pamoja na afya kwa ujumla.

Hata hivyo Bi Juliet Mgasa amesema kuwa shirika hili lilijikita katika kutafuta takwimu kwanza ndani ya miaka miwili na baadae kubaini changamoto mbalimbali zilizopo kwa watu wenye ulemavu ikiwemo ukosefu Wa elimu ya kijinsia kwa wanajamii kwa ujumla.

Aidha nae mjumbe kutoka kamati ya Shivyawata taifa Bw.Elisan Mkude amelishukuru shirika hilo kwa kuwaona watu wenye ulemavu katika mkoa Wa kagera na kuitaka jamii kuelewa maana ya elimu jumuishi kwa watu walio katika makundi maalumu nakutambua thamani yao.

Vilevile nae katibu Wa chama cha watu wenye ulemavu mkoa Wa kagera Bw.Swetbert Mshanga ameitaka jamii kutambua uwepo wao katika jamii na pia kushirikishwa katika maamuzi bila kusahau kupewa elimu jumuishi.

Ameyasema hayo wakati akiwasilisha risala yake kwa mgeni rasimi Afisa elimu mkoa Wa kagera Juma Muiina kwa niaba ya Mkuu Wa mkoa ambapo amezitaja changamoto mbalimbali wanazo kumbana nazo watu wenye ulemavu ikiwa ni kutopewa ushirikiano hata katika ngazi za uongozi na kwa upande Wa wanafunzi miundombinu kutokuwa rafiki pamoja na ukosefu Wa elimu ya awali katika shule zilizo na elimu jumuishi.

Ameongeza kuwa mbali na baadhi ya changamoto hizo yapo mafanikioa walio nayo ikiwa wameweza kutoka mafunzo mbalimbali ya elimu jumuishi kwa baadhi ya wilaya katika mkoa Wa kagera, pia ameuomba uongozi Wa shirika la VSO kwa kushirikiana na mkoa Wa kagera kuweza kupatiwa ushirikiano pamoja na kuwezeshwa kushiriki katika maadhimisho yao ambayo ufanyika December 5 kila mwaka.