Home Mchanganyiko KIKWETE ATAKA WAZEE WAHUSISHWE KUTATUA MIGOGORO YA MIPAKA.

KIKWETE ATAKA WAZEE WAHUSISHWE KUTATUA MIGOGORO YA MIPAKA.

0

*************************************

Na Shushu Joel

MBUNGE wa Jimbo la chalinze Mh Ridhiwani Kikwete ameitaka serikali kuwatumia wazee wa maeneo husika ili kuondoa migogoro ya mipaka baina ya Kijiji na Kijiji au ile ya kata kwani kwao wameishi maeneo hayo kwa kipindi kirefu.

Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wananchi wa jimbo la chalinze ambapo mbunge huyo alisisitiza kuwa endapo wazee wakipewa nafasi ya kutatua migogoro hiyo itabaki kuwa ni historia.

Aliongeza kuwa katika jimbo lake kuna changamoto ya uwepo kwa baadhi ya maeneo kuwa na matatizo hayo hivyo amewashauri wataalamu wa idara ya ardhi kuwatumia wazee wa maeneo husika kwani wanaweza wakawapa mwelekeo wa kujua jinsi ya kumaliza changamoto hizo.

“Nimefanya mikutano katika jimbo langu kwenye vijiji taklibani vyote hivyo mimi kama mbunge nimeshauri kutumiwa kwa wazee ili kutatua changamoto hiyo”Alisema Kikwete.

Aidha aliongeza kuwa kitu kingine ambacho kimekuwa kikiwachanganya wananchi ni maamuzi yanayofanywa na wataalam katika utatuzi wa migogoro hiyo kwa wao kwenda kwenye maeneo na kuwahusisha watu ambao si sahihi.

Kwa upande wake mzee Said Lufunga (79) amempongeza mbunge kwa kutambu changamoto za mipaka ambazo zimekuwa ni kero kubwa katika jamii.

“Ukimuona nyani kazeeka amekwepa mishale mingi hivyo aminini wazee ni kimbilio la matatizo yote” Alisema Lufunga.

Naye Bi, Amina Ramadhani(76) amesema kuwa migogoro inatengenezwa na wataalam kutokana na kutotaka kusikiliza wazawa kwani wao wamekuwa wakitumia vifaa vya kisasa tu.

Hivyo amemuomba mbunge Kikwete kuendelea kulipigia kelele Jambo hili uenda mwafaka ukapatikana.

“Wazee kwa kushirikiana na viongozi wa dini wanaweza wakawa suluhiaho la hili Jambo katika halmashauri yetu ya chalinze ” Alisema.