*******************************
Na Mwandishi wetu Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha mrisho amezindua mpango mkakati wa kibiashara wa wilaya mbili za simanjiro na longido ambao unalenga kuweka mipango ya namna gani wafugaji watajikwamua kiuchumi.
Akizungunza katika warsha ya uzinduzi wa mpango huo uliofadhiliwa na mradi wa Maisha bora kwa ushirikiano wa shirika la Trias Gambo amesema kuwa mpango huo utawezesha wafugaji wa wilaya hizo kuwa na thamani hapa nchini.
Amesema kuwa kupitia mpango huo uliozinduliwa wafugaji wanapaswa kuongeza mnyororo wa thamani ya mifugo yao ili waweze kuzalisha kwa tija na kwa faida tofauti na walivyozoea kufuga kimazoea.
Aidha ameishukuru serikali ya Beljam kwa kutoa kiasi cha dola za kimarekani milioni 11 kuhakikisha mradi huo unatekelezeka katika wilaya za longido na simanjiro.
Nae mkurugenzi wa shirika la Trias afrika mashariki bw Bart Casier amesema kuwa wameamua kushirikiana na serikali ili kuwakwamua kiuchumi wafugaji katika kuhakikisha wanaondokana na changamoto zinazowakabili.
Amesema kuwa mbali na kusaidia miradi hiyo hadi sasa wamefainikiwa kusaidia vikundi vya vikoba 450 kwa kuwakopesha pamoja na vyama vya kuweka na kukopa (sacos) lengo likiwa ni kuwawezesha kujikwamua kiuchumi
Amesema kuwa wanafanya kazi kwa kushirikiana na serikali pamoja na sekta nyingine ili kukomboa jamii kwenye sekta za biashara,lishe,maji pamoja na mitaji.
Kwa upande wake mkuu wa wikaya ya longido frenk Mwaisumbe amewashukuru maisha bora kwa kushirikiana na serikali kwa kuwawezesha mradi huo kwani anaamini utawanufaisha wafugaji lakini pia kuwanufaisha wanawake kwa kuwapatia mikopo
Mwaisumbe alimalizia kwa kusema kuwa bado katika jamii za wafugaji kunawanaofuga kama utamaduni hali ambayo inasababisha washindwe kufikia malengo yao lakini sasa kupitia mkakati huo hali itabadilika