OFISA Programu na Harakati na Ujenzi wa Pamoja kutoka Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Anna Sangai mwishoni mwa wiki wakati wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuripoti habari za jinsia kushoto ni Afisa Habari wa Mtandao wa wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Monica John
Afisa Habari wa Mtandao wa wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Monica John akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo
Sehemu ya waandishi wa habari mkoa wa Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye semina hiyo kulia ni Amina Omari wa gazeti la Mtanzania kushoto ni Khadija Baragasha wa EATV na Majira na George Sembony wa gazeti la Citizen mkoa wa Tanga
Sehemu ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo kulia ni Rais Saidi wa Gazeti la Mwananchi akiwa na waandishi wengine wa mkoa huo.
ATHARI za mfumo dume kwenye jamii ni kubwa sana kutokana na kwamba unagusa maeneo mengi ya kichumi, kijamii upatikanaji wa huduma za jamii huku akieleza jamii inatakiwa kutambua kwamba eneo ambalo kuna hali hiyo hata maendeleo yatachelewa kupatikana.
ATHARI za mfumo dume kwenye jamii ni kubwa sana kutokana na kwamba unagusa maeneo mengi ya kichumi, kijamii upatikanaji wa huduma za jamii huku akieleza jamii inatakiwa kutambua kwamba eneo ambalo kuna hali hiyo hata maendeleo yatachelewa kupatikana.
Hayo yalisemwa na OFISA Programu na Harakati na Ujenzi wa Pamoja kutoka Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Anna Sangai mwishoni mwa wiki wakati wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuripoti habari za jinsia ambapo alisema sababu mfumo unaathiri uchumi na kupelekea maendeleo kushindwa kupatikana .
Akitolea mfano pale wanawake wanapohitaji nafasi ya kushiriki kwenye uchumi unakuta mfumo unaonyesha wanawake hawatakiwi kufanya hivyo na badala yake wanakaa nyumbani kwa hiyo wanapookaa nyumbani kwenye eneo la uchumi umaskini unaendelela kwa sababu wanaamini wanawake wapo wengi zaidi ya asilimia 50 hivyo wanaposhiriki kwenye suala la uzalishaji mali wanaongeza kipato cha familia na Taifa kwa ujumla.
“Hivyo lazima jamii ibadilike na kuacha na mfumo dume ambao umekuwa kikwazo kikubwa cha uchelewashaji wa maendeleo hivyo badala yake waweze kutoa nafasi kwa lengo la kuoindosha hali ya namna hiyo “Alisema
Hata hivyo aliwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi kwenye chaguzi hizo zijazo wanawake popote walipo waone hiyo ni nafasi ya kujitokeza na wafahamu michakato na namna ya kuchukua fomu na kujiandaa kwa ushiriki wao.
“Tuna nafasi kubwa ya kushiriki kwenye uchaguzi hizo zijazo na kushiriki kwa sababu tunaona jinsi Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu anavyotuongoza vizuri inawezekana mwanamke akawa Rais na nchi ikaendelea vizuri kwa sababu ni waadilifu na wachapa kazi “Alisema.
Naye kwa upande wake Afisa Habari wa Mtandao wa wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Monica John alisema kwamba mfumo dume ni mfumo uliopo kwenye jamii na wakati mwengine inatokana na nguvu aliyokuwa nayo mtu katika hali ya kumiliki rasilimali kutoa maamuzi.
Alisema sehemu kubwa kwenye jamii mfumo dume unasababishwa na wanaume wamekuwa wakinyima sauti wanawake katika kuongeza vitu na hata kumiliki rasiliamali lakini pia upo kwenye pande mbili kutokana na kwamba mwisho ya siku unaweza kuathiri pande zote mbili.