
Silvia Mchuruza,Bukoba.
Wizara ya afya jinsia wazee na watoto imetoa semina kwa waandishi Wa habari kuhusu kujikinga na ugonjwa Wa Ebola kutokana na Mkoa huo kuwa eneo la mpakani.
Akizungumza mwasilishaji Wa mada katika wizara ya afya jinsia wezee na watoto Bw.Fadhili Kilamile amesema kuwa ugonjwa huu kwa mara ya kwanza uligundurika mwaka 1979 huko nchini Zaire ambayo kwa sasa ni DRC Congo.
Hata hivyo ameongeza kuwa licha ugonjwa huu kugundurika nchini Congo baadhi ya nchi zingine za afrika zimepata madhara kama vile Sudan ikiwa ni kwa asilimia 53%, na Bundibugyo(Uganda) asilimia 27%.
“Ukubwa Wa virus vya Ebola kwa upande Wa Congo imechua sehemu kubwa sana ambapo uenezwaji Wa ugonjwa huu ni 68% na kati ya mtu 1-10 ufariki dunia kwahiyo ugonjwa huu auna tiba kabisa” aliswema Bw.Fadhili.
Aidha ameongeza kuwa tafiti zilizofanyika march 27 mwaka huu shirika la afya duniani WHO zinaonesha kwamba zaidi ya nchi za ukanda Wa ikweta ndizo zenye hatari zaidi katika maambukizi ya virus vya Ebola na kutaja baadhi ya dalili za ugonjwa huo ambazo ni uchovu,maumivu ya misuli,kuwa na macho mekundu, maumivu ya tumbo na kupanda kwa joto la mwili.
Sambamba na hayo amesema kuwa watu ambao zaidi uathirika zaidi ni wanawake na kuongeza kuwa mgonjwa mmoja utibiwa kwa gharama kubwa zaidi ya million 19 mpaka 20 ambapo mavazi wanayovaa wauguzi Wa ugonjwa huo pia ugharimu kiasi cha shilingi laki tano kwa muuguzi mmoja na kuwataka wananchi kuwa makini na kuepuka kushikana mikono kutokana na ugonjwa huo uenezwa kwa kushikana mikono.