
Bw. Emmanuel Lyimo kutoka Shirika la Utunziaji wa Misitu Tanzania (TFCG)akitoa mada katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu habari za utunzaji wa misitu inayofanyika kwenye hoteli ya Oacis mjini Morogoro kwa siku mbili.


Bi. Bettie Luwuge kutoka shirika la Kuhifadhi Misitu Tanzania (TFCD) akitoa maelezo kwa washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari utunzji wa misitu inayofanyika mjini Morogoro.




Mwandishi Mkongwe wa habari Mwalimu Allan Lawa akitoa mada katika mafunzo hayo yanayofanyika mjini Morogoro.

Mwanasheria Wilson Mukebezi akitoa mada kuhusu sheria na kanuni mbalimbali zinazosimamia uhifadhi wa misitu wakati alipowasilisha mada katika mafunzo hayo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada.

Bi. Bettie Luwuge kutoka shirika la Kuhifadhi Misitu Tanzania (TFCD) pamoja na baadhi ya watoa mada katika mafunzo hayo.
………………………………………………
WAANDISHI wa habari 28 kutoka vyombo mbalimbali vya habari wamepatiwa mafunzo na kuhusu Usimamizi Shirikishi wa Misitu (USM).
Mafunzo hayo yametolewa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Mtandao wa Jamii wa Usimamizi Misitu Tanzania (Mjumita), Shirika la Kuendeleza Nishati Asili Tanzania (TaTEDO) ambayo yanatekeleza Mradi wa Kuleta Mageuzi Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS), chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswis (SDC).
Akizungumzia lengo la mafunzo hayo Mkurugenzi Msaidizi wa TFCG, Emmanuel Lyimo alisema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu rasilimali misitu inavyoweza kutunzwa na kutumika kwa faida ya jamii husika.
Lyimo alisema waandishi wa habari in kiungo muhimu kati ya jamii na watunga sera hivyo wao wanaamini kundi hilo likipata uelewa litarahisisha jamii nzima kuelewa lengo lao.
“Tumekuwa na utekelezaji wa mradi wa TTCS kwa takribani miaka saba sasa hivyo wakati tunatekeleza mradi kwa wananchi waandishi wa habari ndio kiungo sahihi ya kufikisha ujumbe kwa jamii bila kupindapinda,” alisema.
Lyimo alisema wamekuwa wakishirikisha waandishi wa habari kila mara ili kuhakikisha kunakuwepo kizazi ambacho kitadumu kwenye uandishi wa aina hiyo kila wakati.
Alisema walilazimika kuja na mradi huo ili kuhakikisha misitu ya vijiji inakuwa salama na endelevu jambo ambalo limeweza kuonekana kivitendo.
Lyimo alisema mradi wa mkaa endelevu umeweza kufanya mageuzi ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wengi vijijini hivyo waandishi wa habari wakielewa wataweza kufukisha ujumbe kwa haraka.
Alisema misitu ni rasilimali ambayo inaweza kukabiliana na changamoto zilizopo kwa jamii hivyo wamekuwa wakijengea uelewa wanavijiji kuhusu faida za matumizi endelevu ya rasilimali hiyo.
Aidha, Lyimo alisema utafiti umeonesha kuwa misitu mingi inamalizika kutokana na uanzishaji wa mashamba mapya.
Alisema kilimo pamoja na umuhimu wake kwa jamii kimekiwa kikichangia upotevu wa misitu kuliko ukataji wa mkaa hivyo ni jukumu la vyombo vya habari kuonesha hali halisi.
“Tumetembelea wilaya 67 mikoa 22 matokeo yanaonesha ukataji wa misitu unasababishwa na uandaaji wa mashamba mapya na mkaa ni sehemu ndogo hali ambayo inachangia upotevu wa hekta 469, 000 kila mwaka,” alisema.
Mkurugenzi huyo alisema ili changamoto hiyo ifahamike kwa jamii na watunga sera waandishi ndio kiungo sahihi hivyo ni imani yake mafanikio yatapatikana.
Ofisa Wakujengea Uwezo wa TFCG, Simon Lugazo alisema mradi huo umeweza kuchochea mafanikio makubwa ya kiuchumi, kijamii na maendeleo kwenye vijaji vya mradi.
Lugazo alisema hadi sasa vijiji,halmashauri na wanavijiii wamefanikiwa kuingiza zaidi ya Sh.Bil 3 ambazo zimefanikiwa kitekeleza miradi ya maendeleo.
Alisema fedha hizo zimeweza kutekeleza miradi ya afya, elimu, kilimo, maji na uhifadhi wa misitu ukiimarika.
Ofisa Uhusiano wa TFCG, Bettie Luwuge aliwataka waandishi kutembelea vijiji ambavyo vinatekeleza miradi ya uhifadhi ili kujionea.
“Tumekuwa tukisisitiza USM katika vijiji na matokeo chanya yameonekana tunapaswa kueleza jamii faida na hasara ambazo zinaonekana huko,” alisema.
Kwa upande wake Mwandishi wa Habari Mkongwe, Allan Lawa amewataka waandishi wa habari kuwa wabunifu kwa kuandika habari ambazo zinagusa jamii na nchi kwa ujumla.
Lawa alisema iwapo waandishi wa habari watatumia kalamu zao kwa ufasaha watakuwa na mchango mkubwa kwenye sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya jamii.