Home Mchanganyiko MATINDI ATCL: WAHUDUMU WA NDEGE HAWAAJIRIWI ILI KUJA KUFANYA (CUT WALK) KWENYE...

MATINDI ATCL: WAHUDUMU WA NDEGE HAWAAJIRIWI ILI KUJA KUFANYA (CUT WALK) KWENYE NDEGE, WANAAJIRIWA KWA VIGEZO VYA KIMATAIFA ILI KUHUDUMIA ABIRIA

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la tanzania ATCL Injinia Ladslaus Matindi akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao mkauu ya shirika hilo Posta jijini Dar es salaam leo, kutoka Kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano wa Shirika hilo Bw.Josephat Kagirwa katikati ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Albinus Manumbu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la tanzania ATCL Injinia Ladslaus Matindi akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao mkauu ya shirika hilo Posta jijini Dar es salaam leo, kutoka Kulia ni Meneja Masoko Bi. Christina Tungaraza, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Patrick Ndekana na kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Albinus Manumbu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la tanzania ATCL Injinia Ladslaus Matindi akiakifafanua masuala mbalimbali kwa waandishi wa habari.
…………………………………………………..
Shirika la ndege la (ATCL) limetoa muongozo wa kuzingatia kwa ajili ya kuwapata wahudumu wa ndani ya ndege na kukana ushauri uliotolewa na mmoja wa wabunge wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba wahudumu hao hawana mvuto kufanya kazi katika ndege za shirika hilo.
Akizungumza na Wanahabari leo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Mhandisi Ladslaus Matindi amesema kuwa wao kama Mamlaka wamekuwa wakifuata sheria na vigezo vya  kimataifa mamlaka za usafiri wa anga za kimataifa  zimeweka hivyo wao huzingatia uwezo wa kufanya kazi,uelewa pamoja na haiba hasa urefu usiopungua futi 5.2 kwani kuna vifaa anaweza kuvifikia vikiwemo vifaa va kuhifadhia mizigo pamoja na vifaa vya vya kiusalama.
“Kwa kufuata sheria  za Kimataifa na ambazo tumejiwekea kama (ATCL) muhudumu asiwe na urefu chini ya futi 5.2 na hili tunalifanya makusudi kwasababu tunavifaa ambavyo kwa urefu huo tunahakikisha watavifikia. Na sio vifaa tu vya kuwekea mizigo kama wanavyozungumza watu, kuna vifaa vya kiusalama pia kwani kunaweza kutokea bahati mbaya tatizo lolote je, anaweza kufanya shughuli zake bila tatizo?”. Amesema
Amesema kuwa wahuduma ndani ya ndege wanatofautiana kwani wapo kimadaraja tofautitofauti hivyo madaraja yao yanapanda kadri uwezo na muda aliodumu katika huduma ambayo anayoifanya unavyozidi kama unavyoujua ukichanganya wahudumu ambao ni wazoefu na vijana unao uwezo wa kutengeneza wahudumu wengine wa baadaye wakati hawa wakongwe watakapostaafu na kuondoka kwenye utumishi wao.
“Jukumu la muhudumu si kufanya (Cut Walk) kwenye ndege kama vile yuko kwenye onesho la mavazi au urembe kazi yake kubwa ni kutoa huduma nzuri inayoridhisha kwa wateja wanaosafiri lakini pia ni kuhakikisha usalama wa abiria pamoja na usalama wa ndege hivyo hufundishwa pia kuhusu utoaji wa huduma ya kwanza (First Aid)”.Amesema Injinia Matindi.
Ameongeza kwamba hakuna mhudumu wa nduee za (ATCL) ambaye ameajiliuwa bila kufuata sheria, Kanuni na Utaratibu  wa kimataifa unaosimamia ajira za wahudumu wa ndege na ili muhudumu wa ndege kupata leseni lazima akidhi vigezo vilivyowekwa.