****************************
Na Silvia Amandius.
Bukoba.
Mkuu Wa wilaya ya Bukoba Bw.Deodatus Kinawilo amewaonya watumishi wa Umma kutumia fedha zinazotolewa kwa ajili ya utekeleza Wa miradi inayo wanufaisha wananchi.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na madiwani katika baraza la madiwa ambapo lilikuwa ni baraza la kuwasirisha utekeleza Wa miradi kwa muula Wa kwanza Wa robo mwaka katika halmashauri ya wilaya ya bukoba manispaa.
Amesema kuwa kumekuwepo na ubabaishaji katika utekerezwaji Wa miradi mbalimbali licha ya miradi mingine kukamilika lakini watumishi wengine wamekuwa wakichelewesha maendeleo ya wilaya hiyo.
Pia amezungumzia miradi Wa ujenzi Wa dhahati ya zamzam katika wilaya hiyo kuwa uligharimu jumla ya million 400 ambapo mradi huo ulikamilika kwa wakati na kusimamiwa kwa uangalifu zaidi.
“Kuna watumishi wengine wapo makini katika kusimamia fedha za umma lakini watumishi wengine wanazunguka tu wanapindish pindisha mambo tu sasa niwaambie waheshimiwa madiwani awamu hii ya tano aitaki longolongo inataka kuwatumikia wananchi tu tufanye kazi kwa weredi mkubwa” Alisema DC kinawilo.
Aidha ametoa angalizo kwa watumishi Wa umma kutozitumia vibaya fedha za wananchi kwa sababu in kodi zao na kuwataka watumishi kushirikiana vyema na wananchi Wa wilaya ya halmashauri ya bukoba manispaa.
Hata hivyo ameongezea na kusema kuwa miradi yote ya ukarabatiwa Wa shule ya Bukoba Sekondali iliyopigwa na tetemeko unatakiwa kumarizika kwa wakati sahihi maana serikali imetoa fedha Kamili kwa ajili ya utekelezaji huo ikiwa nizaidi ya 1.4 bilioni zilizotolewa kwa ajili ya ukarabati huo.
“Nitoe lai chondechonde mnapowapa mikataba wakandarasi wasimamieni kwa umakini wamalize miradi kwa wakati kwa ajili ya wananchi na fedha za awamu ya tano zikishaletwa zinaakiwa kutumika kwa wakati sahihi” Alisema DC kinawilo.
Attachments area