Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza weledi katika kazi wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za Kampuni ya mbolea Tanzania-TFC iliyopo Masaki Jijini Dar es salaam leo tarehe 8 Novemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza jambo na Menejimenti ya kampuni ya Mbolea Tanzania – TFC kabla ya kikao kazi na watumishi wa kampuni hiyo iliyopo Masaki Jijini Dar es salaam leo tarehe 8 Novemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akipitia taarifa, sheria na muongozo wa kampuni ya Mbolea Tanzania – TFC kabla ya kikao kazi na watumishi wa kampuni hiyo iliyopo Masaki Jijini Dar es salaam leo tarehe 8 Novemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na watumishi
wa kampuni ya Mbolea Tanzania – TFC wakati wa kikao kazi na watumishi hao
kilichofanyika eneo la Masaki Jijini Dar es salaam leo tarehe 8 Novemba
2019.

Na Mathias Canal,
Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameivunja Bodi
ya Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) iliyoteuliwa rasmi tarehe 1 Disemba 2017
ikiwa na wajumbe sita ambao ni Mhandisi Eli Pallangyo, Bw Nuru Ndile, Bi
Rosemary Msabaha, Bw Peter Shao, Dkt Kadida Mashaushi na aliyekuwa Mwenyekiti
Marehemu Prof Egid Mubofu.

Waziri Hasunga amefanya maamuzi hayo leo tarehe 8
Novemba 2019 wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za Kampuni hiyo
ya TFC zilizopo Masaki Jijini Dar es salaam huku akimuhamishia Wizarani Meneja
Mkuu wa Kampuni hiyo Ndg salum Mkumba ili kumalizia mkataba wa mwezi mmoja
uliosalia.

Amesema kuwa Meneja huyo anatakiwa kuripoti Wizara ya
Kilimo Jijini Dodoma kuanzia kesho tarehe 9 Novemba 2019 huku akieleza kuwa
nafasi yake itasalia bila uteuzi mpaka atakapotoa maelekezo mengine.

Akizungumza katika kikao hicho Waziri Hasunga amesema
kuwa ameivunja Bodi hiyo kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kuagiza
mbolea kutoka nje ya nchi hivyo kusababisha kampuni kushindwa kufanya biashara,
kampuni kujiendesha kwa hasara hivyo kushindwa kufikia matakwa ya kuanzishwa
kwa kampuni hiyo ya kuwa msambazaji kiongozi na anayeaminika kwa mbolea ya
pembejeo zingine nchini kwa kuzingatia mahitaji ya mazao na afya ya udongo.

Kadhalika amesema kuwa Bodi hiyo pamoja na Meneja Mkuu
imeshindwa kutekeleza wajibu wake ili kutoa suluhisho sahihi lenye gharama
nafuu ya mbolea kwa wakulima na kwa wakati kwa kuzingatia hali ya udongo kwa
mujibu wa Dira na Dhima ya Kampuni hiyo. Mengine ni kushindwa kuifufua na
kuiendeleza kampuni hiyo

Kwa upande wa watumishi wengine wote waliobaki Waziri
wa Kilimo amewapa wiki mbili kuhakikisha kuwa mbolea zilizopo bandarini zaidi
ya makontena 127 ziwe zimetoka na kuwafikia wakulima kote nchini. “Tunahitaji
mbolea lakini hiyo mbolea imekaa bandarini hivyo haraka iwezekanavyo ziende kwa
wakulima” Alisisitiza Mhe Hasunga

Pia ametoa wiki moja kwa wafanyakazi hao kumpatia
mabadiliko ya mtaji wa kampuni ili uendane na viwango vinavyotakiwa kwa mujibu
wa sheria za makampuni hapa nchini, kuainisha mpangokazi unaoonyesha namna
watakavyopata mbolea na kuisambaza mwaka huu, namna ya kusambaza viuatilifu na
jinsi ya kuvipata vingine, kadhalika namna watakavyoisaidia serikali katika
usambazaji wa mbegu na pembejeo nyingine.

“Ndani ya muda huo mkiniabia mmeshindwa nitajua
hamuwezi kufanya kazi hivyo nitawapa kazi watu wengine ambao wengi wapo mtaani
hawana kazi na wanaweza kufanya kazi hizo” Alisema

Waziri Hasunga amesema kuwa alimpatia maelekezo Meneja
Mkuu wa kampuni hiyo ya mbolea (TFC) ya kutafuta eneo kwa ajili ya kujenga
mtambo wa kuchanganyia mbolea lakini mpaka sasa Taasisi hiyo imeshindwa
kutafuta eneo hilo kwa kipindi cha karibu miezi 9.

Katika hatua nyingine Waziri Hasunga amesema kuwa ataagiza
wakaguzi maalumu kuikagua kampuni hiyo hususani kwenye majukumu ya kiutendaji
kuangalia chanzo cha kushindwa kutekeleza majukumu yake na hatua zitachukuliwa
kwa matokeo yatakayobainika.

Kadhalika amesema kuwa ametengua uteuzi wa Mrajis wa
Vyama vya Ushirika Ndg Tito Haule, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania
Ndg Primus Kimaryo, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Tumbaku Dkt Julius Ningu wote
kwa pamoja ni kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao.

Waziri Hasunga amewataka watendaji hao kubadilika
katika utendaji kazi ili kuongeza ufanisi na tija katika sekta ya kilimo ili
kuwa na usalama wa chakula na kutofanya kazi kwa mazoea.