Meya wa Manispaa ya Mpanda William Mbogo akizungumza katika Baraza la madiwani wa manispaa hiyo.
Baadhi ya Madiwani wa Madiwani wa Manispaa ya Mpanda wakifuatilia hoja katika kikao cha Baraza.
*************************************
Na Mwandishi wetu, Katavi
Meya wa Manispaa ya Mpanda William Mbogo amelishukuru Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kujitoa kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Majengo
Ametoa shukrani hizo katika Baraza la Madiwani wa halmashauri ya Manispaa hiyo ambapo amesema Shirika hilo limetoa mifuko 100 ya saruji pamoja na bando moja ya bati
Amesema kufuatia msaada huo wadau mbalimbali wameendelea kujitokeza kuchangia ujnzi huo, ambapo wazazi wamechanga kiasi cha 5,000/- kila mmoja, na imepatikana jumla ya shilingi 236,000 katika kuunga mkono juhudi za ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika madarasa
Aidha wadau na wabunge wa mkoa wa katavi nao wamechangia kwa namna mbalimbali katika kuhakikisha watoto wanasoma katika mazuri
Amewataja waliochangia kuwa ni pamoja na mdau Kevin Mbogo ambaye ametoa kiasi cha shilingi 500,000/- kwa ajili ya maji ya kumwagilia tofali, mbunge wa jimbo la Mpanda Kati Sebastian Kapufi ametoa 500,000/- kwa ajili ya ujenzi wa vyoo, na mfuko wa jimbo umetoa shilingi 1,000,000/-; mbunge wa viti maalum Anna Lupembe ametoa printa moja na Tusker Mbogo mbunge wa viti maalum ametoa shilingi 500,000/- kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa choo
Ameongeza kuwa mpaka sasa wana tofali 2,700 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa