Home Mchanganyiko KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI, PHAUSTINE KASIKE ATEMBELEA MRADI WA KOKOTO GEREZA...

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI, PHAUSTINE KASIKE ATEMBELEA MRADI WA KOKOTO GEREZA MSALATO, MKOANI DODOMA

0

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua moja ya eneo la kulipulia mawe ya kokoto katika eneo la Gereza Msalato leo alipofanya ziara ya kikazi.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) akiongea na Wafungwa wa Gereza Msalato(hawapo pichani) wanaofanya kazi za uzalishaji kokoto katika mradi huo wa Gereza hilo. Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Keneth Mwambije.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) akiangalia mtambo wa uzalishaji katika mradi wa uzalishaji kokoto wa Gereza Msalato, Dodoma leo alipofanya ziara ya kikazi. Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza(SHIMA) limewekeza mradi huo wa kokoto katika eneo la Gereza Msalato, Mkoani Dodoma.

Mkuu wa Gereza Msalato, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Huruma Mwalyaje(katikati) akimwelezea jambo Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) kabla ya kutembelea eneo la mradi wa uzalishaji kokoto. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi
wa Magereza, Keneth Mwambije(Picha zote na Jeshi la Magereza).

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) akiangalia kokoto zinazozalishwa katika mradi huo wa Gereza Msalato leo alipofanya ziara ya kikazi. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Keneth Mwambije na Kulia ni Mkuu wa
Gereza Msalato, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Huruma Mwalyaje.