Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Anitha Msangi (wa tatu kulia) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza maandalizi ya Taifa Stars kuelekea mechi yake ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) dhidi ya Equatorial Guinea. Wa kwanza kulia ni Haji Manara, mwenyekiti wa kamati ya uhamasishaji akifuatiwa na Katibu Mkuu wa TFF Kidau Wilfred na wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa Stars supports, Godson Karigo.
Katibu Mkuu wa TFF Kidau Wilfred (kulia), akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza maandalizi ya Taifa Stars kuelekea mechi yake ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) dhidi ya Equatorial Guinea. Kulia kwake ni Meneja Masoko wa kampuni ya Bia ya Serengeti Anitha Msangi akifuatiwa na Haji Manara, mwenyekiti wa kamati ya uhamasishaji na Cliford Ndimbo, Afisa habari wa TFF.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari, wakifuatilia mkutano wa kutangaza maandalizi ya Taifa Stars kuelekea mechi yake ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) dhidi ya Equatorial Guinea utakachezwa jijini Dar es Salaam November 2019.
Mwenyekiti wa kamati ya uhamasishaji ya Taifa Stars Haji Manara (wa pili kulia) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza maandalizi ya Taifa Stars kuelekea mechi yake ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) dhidi ya Equatorial Guinea. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF Kidau Wilfred akifuatiwa na Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Anitha Msangi Na kushoto ni Afisa habari wa TFF Cliford Ndimbo.
………………………..
Na Mwandisdi Wetu
Mdhamini mkuu wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries (SBL) kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager, imeahidi kuendelea kuwapa raha wapenzi wa soka hapa nchini kupitia udamini wake kwa Timu ya Taifa.
Taifa Stars, inatarajia kucheza mechi yake ya kufuzu tiketi ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) dhidi ya Equatorial Guinea Novemba 15 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kutangaza maandalizi kuelekea mechi hiyo, Meneja Masoko wa SBL Anitha Msangi alisema SBL kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager ipo bega kwa bega na Timu ya Taifa pamoja na mashabiki wa soka.
“SBL kupitia bia yetu ya Serengeti Premium Lager tutataendelrea kuwapa burudani mashabiki wa soka kwa kuhakikisha tunaiwezesha timu yetu ya taifa kufanya vizuri lakini pia kupitia bia ya Serengeti kuwafanya mashabiki wafurahie mechi pamoja na bia yao pendwa,” alisema
Anitha alisema, ili kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanafurahia mechi hiyo, kampuni ya SBL itaweka skirini kubwa sehemu mbali mbali ambazo zitaonyesha mechi bure huku nafasi ya kufurahia bia ya Serengeti ikitolewa.
“Tujitokeze kwa wingi kuishangia timu yetu huku tukifurahia bia yetu ya Srengeti Premium Lager ambayo ni fahari yetu,” alisema
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Kidau Wilfred alisema timu itaingia kambini hivi karibuni kujiandaa na mchezo huo wa nyumbani..
Kidau alifafanua kuwa, mchezo wa pili wa kufuzu AFCON utachezwa ugenini ambapo Stars wataenya na Libya Novemba 19,2019, siku 4 tu baada ya kucheza mchezo wa kwanza.
“Tunawaomba Watanzania kwa pamoja tuungane kwa ajili ya timu yetu ya Taifa. Tujitokeze kwa wingi siku ya mechi na kuishangilia kwa nguvu zetu zote ili kuwapa hamasa wachezaji wetu waweze kufanya vizuri,” alisema Ndimbo.