Home Michezo SAMATA AWEKA REKODI YAKE ANFIELD

SAMATA AWEKA REKODI YAKE ANFIELD

0

*********************************

NA EMMANUEL MBATILO

Ni usiku mwingine wa Ulaya ambao mtanzania Mbwana Ali Samatta anaechezea klabu ya KR Genk ya nchini Ubeligiji alijiandikia rekodi yake ya kuwa mtanzania wa kwanza kuifunga timu ya Liverpool, vile vile kuwa mtanzania wa kwanza kufunga goli ndani ya uwanja wa Anfield.

Samata alipata bao hilo kupitia mpira wa kona na kuweza kuisaidia klabu yake kwenda mapumziko wakiwa 1:1 lakini baadae Liverpool iliweza kupata bao lingine katika kipindi cha pili na kufanya mechi kuisha kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa 2:1.

KR Genk imeshindwa kufanya vizuri katika kundi lake hivyo wanasubiri kukamilisha ratiba tu kwani pointi walizonazo haziwezi kufikia timu za juu mbili ambazo zitakwenda moja kwa moja katika hatua nyingine.